Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Kustawisha hisia na jinsi ya kuishi na watu wengine

Muache mtoto aweze kujitegemea. Wakati wanapoanza shule; watoto wanatakikana kuchagua nguo na kujivalia nguo wenyewe, kupiga meno mswaki, kujisafisha wenyewe na kadhalika. Usijaribu kuwafanyia kila kitu kwa sababu inaonekana rahisi na haraka.

Msikilize mtoto wako. Furahishwa na anachosema, na anapoulizia maoni kuhusu vitu. Wacha mtoto wako achague mtakacho kula usiku (peana chaguo na muache achague moja). Kwa njia hii watajifunza kusema kusema mambo muhimu.

Mfunze mtoto wako kuwa na jukumu kwa matendo yake. Mtoto wako akifanya makosa, lazima ayabebe na jukumu lake. Hakikisha mtoto wako anaelewa ni kitendo usichokipenda, lakini si yeye. Kwa mfano, usiseme, ”wewe ni msichana mtundu”. Badala mwambie “Hicho ni kitendo kibaya umefanya”

Jivunie mafanikio ya mtoto wako. Onyesha michoro na kazi yake nyumbani kwako, wapigie simu familia uwambie anapofanya vizuri katika michezo. Wacha mtoto wako ajue kwamba unajivunia akifanya vyema, na hata akitia bidii.
 


0
No votes yet
Your rating: None