Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Kukuza maumbile

Mtoto wako anafaa kuwa na misuli mizuri ili aweze kukaa, kumakinika na kutumia penseli akiwa darasani.

Ujuzi wa misuli minene


‘Gross Motor Skills’ ni vitendo vinavyo dhibitiwa na misuli mikubwa ya mwili kama vile kuweza kutembea, kukimbia na kuruka. Unaweza msaidia mtoto wako kujenga uwezo huu kwa: Kucheza mpira na mtoto wako. Mhimize mtoto wako kurusha na kunyaka mpira wa maharagwe au mpira mdogo.

Msaidie mtoto wako kusimama na vidolevya miguu. Ajifunze kupimisha. Mfunze kutembea kwenye ukuta mwembamba ama matofali kidogo yamepangwa. Akiweza kutembea bila shaka, mwambie atembee kinyumenyume halafu ashike mpira akiwa amejipimisha. Fanya mazoezi ya kurukahika, churachura na kubingiria na mtoto wako.

Ujuzi wa misuli laini


‘Fine Motor Skills’. Hizi zinadhibitiwa na misuli midogo, na hizi ni uwezo wa kuchukuwa vitu vidogo na kushikilia penceli. Naweza msaidia mtoto wako kujenga huu uwezo kwa kumpa mazoezi yafuatayo:

Kutengeneza mipira midogo ya kucheza – donge kwa kulisokota katikati ya vidole na gumba. Kukata picha kwa kutumia makasi madogo
Kurarua magazeti ama makaratasi kuwa kambaa ama kuisokota kuwa mipira midogo
Kutunga shanga ama mirija kwenye uzi. Kuchora na kupaka rangi

1.5
Average: 1.5 (2 votes)
Your rating: None