Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Makuzi ya mazungumzo na lugha

Mtoto wako anawezakuwa mpayukaji ama mkimya zaidi na mwenye kutafakari. Vyovyote vile, kuwa na uwezo wa kuwasiliana ni muhimu sana. Unaweza msaidia mtoto wako kujenga ujuzi wa lugha kwa:

  • Kutotumia ‘usemi wa kitoto’. Wafundishe watoto majina sahihi ya vitu na uwaongeleshe sawa na waziwazi.
  • Kuzungumzia siku yake. Jaribu kuweka kando muda mfupi kila siku umuulize kuhusu vitu alivyofanya mchana.
  • Mpatie vitendawili na muimbie nyimbo za nasari pamoja.
  • Mfafanulie vitu mtoto wako na mwambie akufafanulie vitu.
  • Muulize vitu kama: Huu mti ni mfupi au mrefu?
  • Hiki kitambaa ni laini au chakwaruza? Hichi kitu ni kigumu au laini? Ni moto au baridi?
  • Mwanzie hadithi mtoto wako halafu mwambie akumalizie au afafanue tukio.

 

0
No votes yet
Your rating: None