Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Utajaji wa Nambari/Utakwimu

Ujuzi wa nambari ni mhimu katika maisha, na mtoto wako lazima awe na msingi anapoanza shule. Mtoto wako anahitaji kujua vipengee vifuatavyo:

Kuhesabu: Kuhesabu kwa sauti (angalau hadi ishirini)


“Ordinals:” Kufahamu nafasi ya vitu katika mshororo, kama vile kwanza, pili, tatu na kuendelea.


Mfuatano: Kuwa na uwezo wa kupanga vitu kwanzia kidogo hadi kikubwa na kinyume


Ulinganisho: Kuweza kuweka nambari sahihi ya kitu / chombo kwa nambari iliyoandikwa. Kwa mfano kuweka shanga tano kwa nambari tano.
Uwezo wa kunakili: Kuingalia michoro, kuichora na baadaye kuhusisha sifa zote zitambulikanazo.


Kuweka kwa vikundi: Kuweza kupanga vitu tofauti katika vikundi vilivyosawa na sawia.


Msaidie mtoto wako kujenga ujuzi huu kwa:

  • Kuhesabu vitu pamoja kwa mfano: Miti mingapi iko kiwanjani? Watoto wangapi wanacheza nje? Tunahitaji vijiko vingapi tuandae mezani?
  • Kuhesabu pamoja 1 hadi 20 (ama 50, ama 100 – utashangaa vile anavyofanya vizuri)
  • Muonyeshe mtoto wako nambari zilizoandikwa na umsaindie kuzifahamu. Anza tu na 1 hadi 10.
  • Mukitazama makundi ya vitu na mtoto wako, mwambie mtoto wako akueonyeshe ni gani iko katika nambari tatu katika mshororo au tano au tisa.
  • Mwambie mtoto wako akusaidie kufananisha soksi zako unapofua, mwambie akwambie ni soksi ngapi ziko pale na peya ngapi ziko pale zikikunjwa.
  • Jizoeshe msingi wa kujumlisha na kuondowa na mtoto wako kwa mfano: Ukiwa na biskuti mbili na nipeane moja, nitabaki na ngapi? Ukiwa na peremende tano na ule tatu, utabakisha ngapi?
  • Tengeneza choro na shanga kwenye uzi, au uchore moja halafu umwambie mtoto wako aigize.
     

 

 

 

0
No votes yet
Your rating: None