Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Ujenzi au taratibu za fikira

Mtoto wako anahitaji kufahamu na kuelewa:

Rangi: Mfunze mtoto wako kufahamu rangi msingi (nyekundu, majano na samawati) na rangi za upili (rangi ya biriani - orange, rangi ya kijani kibichi - green na rangi ya zambarau - purple.). Lazima aelewe kwamba rangi za upili zinapatikana kwa kuchanganya rangi za msingi pamoja (Nyekundu manjano = rangi ya biriani, manjano samawati = kijani kibichi; nyekundu samawati = zambarau).

Umbo: Mfunze mtoto wako kufahamu na kutaja majina duara, mraba, pembe tatu, mstatili, duara yai, nusu duara, pembe sita, nyota. Unaweza kuunda mchezo wa kuona na kutambua kila umbo utakaloliona ukiwa matembezi au garini.

Kiwango: Msaidie mtoto wako afanye mazoezi ya kutambua saizi tofauti. Ongea kuhusu ndogo, ndogo kiasi, ndogo zaidi na kubwa, kubwa kiasi, kubwa zaidi. Muulize mtoto wako ni nani aliye mrefu zaidi katika familia yenu na ni nani aliye mfupi zaidi. Mkitazama picha za wanyama, muulize yupi ni mkubwa zaidina gani mdogo zaidi, yupi mwenye mkia mrefu zaidi na yupi mwenye mfupi zaidi.

Maumbile Asilia: Wacha mtoto wako ahisi tofauti ya maumbile asilia ya vitu na asimulie anavyohisi na maneno atakayotumia kufafanua. Shina la mti ni laini au lina mkwaruzo? Je ngozi ya mbwa ni laini au ya dungadunga. Jiwe ni gumu, pamba ni laini na mengineo.

Wakati: Kujifunza kusoma wakati ni ngumu kwa watoto wadogo. Lakini ongea nao kuhusu wakati na uwaonyeshe saa za ukuta na za mkononi. Unaweza kumwambia wakati wake wakulala ni saa moja na nusu, na hivyo basi atakuwa na chakula cha mchana saa saba kamili na chakula cha jioni saa kumi na mbili kamili. Unaweza kumfuza kuhusu jana, leo na kesho na kuhusu asubuhi, mchana na jioni. Anahitaji kujua siku za wiki / juma, na miezi ya mwaka. Nyimbo zinaweza saidia watoto kukumbuka majina ya siku na miezi na mpangilio yake.

4
Average: 4 (1 vote)
Your rating: None