Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Viazi Vitamu

Viazi vitamu ni mmea ambao kwa kawaida una msimu mmoja. Mmea huu unapandwa kote Afrika ya Mashariki kwenye mashamba madogo madogo kwa ajili ya chakula cha nyumbani au unazidi kupata umaarufu pamoja na vyakula vingine vya kienyeji. Mzizi ya mmea huu huliwa baada ya kuchemshwa au kuchomwa ama pia unaweza kuliwa na vyakula vingine kama, maziwa,uji,supu ama nyama,majani machanga hutumiwa kama mboga. Mmea wa viazi vitamu ni wenye manufaa na wenye madini wengi ukitumiwa kama chakula cha mifugo haswa wakati wa msimu wa kiangazi.kuna aina za mmea huu ambazo zinafaa kwa matumizi haya na kuzaa majani mengi.

Kati ya aina tofauti tofauti za viazi vitamu vinavyokuzwa, kuna aina mbili ambazo zinatambulika pakumbwa. Aina hizi hupandwa katika tropiki zote,na kwa kawaida huwa na rangi nyeupe,nyekundu ama zambarau,hata hivyo aina zenye rangi ya majano zinazidi maarufu makumbwa barani afrika na asia. Aina yenye rangi ya orange, kwa kawaida huwa na kiwango cha juu cha sukari na vitaminiA na kiwango cha chini cha ukuaji. Wataalamu wa afya ya lishe kote Afrika mashariki wanahimiza utumishi wa viazi vitamu vyenye nyama ya manjano ili kupambana na kukithiri kwa ukosefu wa vitamin A ambayo hupunguza kinga ya watoto dhidi ya magonjwa ya kuambukiza yanayochangia pakubwa kwa vifo vya watoto wachanga.majani ya mmea michanga ya viazi vitamu hutumia kama mboga ya kijani kibichi katika baadhi ya nchi na yana wingi wa protini na B-carotene, Thiamine (vitamin b1), Viboflavine(b2), Asidi ya Folic na Ascorbic.

Reference : Infonet-BioVision Office at ICIPE Nairobi

1
Average: 1 (1 vote)
Your rating: None