Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Unawezaje kusoma sasa (ama hivi punde)

Kuna njia za kujimudu kupata masomo na kukusaidia kulipa mahitaji mengine hata kama wewe ni mwanafunzi anaanza masomo karibuni ama anayendealea na masomo. Kwa mipango mingine, yategemea na uwezo wako wa fedha. Inaweza pia tegemea matokeo na gredi ya mwanafunzi.

Usaidizi wa fedha
Kwa mpango wa usaidizi wa bure wa fedha, unapatiwa pesa kujisaidia kulipia mahitaji ya elimu ya juu. Hauhitaji kurudisha pesa unapozipokea.

Scholarship au Msaada wa Masomo
Ni aina ya msaada wa masomo unaopeanwa kusaidia wanafunzi waliofaulu (walio na gredi nzuri shuleni), walio na mahitaji ya fedha na wanaojihusisha na michezo au uigizaji au na mahitaji mengineo

Basari au Usarifu
Msaada wa masomo unapatiwa kulinga na ustahiki na uhitajikaji wa fedha. Masharti ya usarifu yanatofautiana, baadhi hazikushikilii na nyengine zina kuhitaji utumikie kampuni iliyokufadhili baada ya kumaliza masomo.

Mkopo wa Elimu
Wanafunzi wanaomba mikopo ya elimu kuwasaidia kulipia masomo yao ya juu.

Njia nyingine za kufanya masomo kuwa rahisi

Msaada wa fedha, mkopo wa elimu, msaada wa masomo zinasaidia familia na wanafunzi kulipa karo za vyuoni. Pata mengi kuhusu mpango huu kwa mwalimu wako wa ushauri na uelekezaji, maktaba za uma, au afisi yoyote yausaidizi wa fedha katika taasisi yako uliochagua.

Lakini kuna njia zingine za kufanya masomo kuwa rahisi, hasa familia ombao hawapendi kuchukua mkopo. Haya ni yale ambayo wanafunzi wangefanya kupata masomo yao ya juu.

Baki nyumbani
Pengine unasafiri kupa mafunzo ya ujuzi unaotaka, baki na familia yako unaposoma kupunguza gharama ya karo ya makaazi. Ukitaka kukaa mbali na nyumbani tafuta chaguo lililo rahisi kuliko makao yako binafsi kama vile kushiriki na mtu mwingine au kuishi na jamaa wako.

Fanya kazi ukiwa bado unasoma
Kwa kufanya kazi kwa muda wakati unasoma, kutakusaidia kulipia gharama zingine. Unaweza kusoma masaa machache au usome elimu kwa njia ya posta (distance learning)

Kutana na mwelekezaji (counselor) katika ofisi ya usaidizi wa kifedha katika chuo chako.
Chuo chako kinaweza kukupatia maelezo zaidi kuhusu mipango ya usaidizi wa fedha. Hakikisha umekutana na mwelekezaji wa kifedha ili akujulishe ni mipango gani ya usaidizi wa kifedha iliyoko.
 


0
No votes yet
Your rating: None

Ahsante sana.

»