Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Jinsi wakulima wanaweza kuteka maji zaidi katika mashamba yao

Wakulima wanaweza kupunguza gharama za unyunyizaji kwa kupata njia za kukusanya maji ya mvua katika udongo na kuyafanya kupatikana kwa urahisi kwa ajili ya mimea.Zifuatazo ni njia sita za kuwahimiza wakulima watumie maji ya mvua wanayopata kadri  inavyowezekana, na kufanya majaribio ya mbinu za kuvuna maji zinazopunguza kasi ya mwendo wa maji na kuyateka katiika shamba.  

Wakulima wanahitaji maji zaidi kwa mimea yao.Ili kuteka maji zaidi kunafaa kuweko njia za kuzuia maji kupotea kutoka shambani.Kiifaa cha kwanza kinachohitajika ni utazamaji na ufahamu wa udongo na maji.Utazamaji huu unaweza kufanywa kwa kujiuliza maswali yafuatayo:

  • Ni njia gani maji huja shambani? 
  • Maji hutiririka hadi wapi? 
  • Je maji hutiririka hadi katika sehemu ambazo mimea huyatumia? 

Ikiwa maji hayatiririki hadi katika maeneo yanayohitajika,njia za kuyapata na kuyageuza mkondo.Mbinu yoyote ikitumiwa,kumbuka ya kwamba lengo la mwisho ni kuhakikisha maji yanayopita juu ya ardhi yanapata nafasi ya kujikusanya na kuvuja hadi ndani ya udongo.

Kutumia vizuizi kuzuia ama kupunguza kasi ya mtiririko wa maji

Utekaji na ukusanyaji wa maji unawezekana mahali ambapo maji yamezuiliwa kukimbia kutoka shambani.Kufanya hili:

  • Zuia maji kukimbia kwenye sehemu ya juu ya ardhi.

AMA

  • Punguza mwendo wa maji ili yasibebe udongo. 

Mtiririko wa maji unaweza kusimamishwa kupitia matumizi ya vizuizi.Vizuizi ni vitu kama contour ridges na mashimo,miyaa na matuta ya mkingamo.Vizuizi hivi vyote hupunguza kasi ya mtiririko wa maji yanapoenda chini ya mlima na kuyapatia wakati wa kuvuja ndani ya udongo.Kufunika udongo kila wakati. 

Moja ya njia wakulima hupoteza maji kutoka kwenye udongo ni kupitia mvukizo.Maji kutoka katika udongo huvukizwa kwenye hewa kabla ya kupata nafasi ya kuvuja ndani ya udongo.Lakini ukifunika udongo,hili halitafanyika.Udongo unaweza kufunikwa na mimea inayoishi,ama na rusu ya mtandazo.

Mtandaazo na majani yaliyo hai huteka maji yanayoanguka ardhi na huyashikilia ili kuyapatia mda wa kuvuja pole pole ndani ya udongo.

Mashimo ya kupanda

Wakulima katika sehemu mingi za Afrika hutumia mashimo ya kupanda.Na wana mafanikio makubwa na mbinu hii.Kuna aina tofauti ya mashimo na wakulima huyatumia kwa njia tofauti.Wakulima wengi huchimba mashimo katika mashanmba yao wakati wa msimu wa kiangazi.Huyajaza na mbolea.Wakati mvua huja,wakulima hupanda nafaka zao katika haya mashimo.Wanasema ya kwamba mimea hukua kwa haraka katika mashimo haya.Hii ni kwa sababu maji hulowa kwa urahisi ndani ya shimo na  hujikusanya hapo ambapo mmea unaweza kuyatumia.Pia,mbolea katika shimo huwa ni mbolea kwa mmea.Kwa maneno mengine,mashimo ya kupanda hukusanya maji na virutubishi mahali ambapo mimea inavihitaji.  

Cross ridging

Saa zingine,mvua inaponyesha,maji mengi huanguka katika mda mfupi na kwa hivyo hayawezi kuzama ndani ya udongo papo kwa hapo.Na huelea mbali.Baadhi ya wakulima 

katika maeneo kame hutumia mbinu spesheli za kuyazuia maji ya mvua shambani mwao.

Wakulima hawa hupanda mimea kama mahindi,mtama,ama na viazi vitamu kwenye sehemu ndefu zilizoinuka.Mvua inaponyesha ,maji hujikusanya katika mitaro baina ya sehemu hizi ndefu zilizoinuka.Ili kuhakikisha maji yanakaa ndani ya mitaro,mkulima hutengeneza vizuizi vidogo vinavyoitwa ‘‘cross-ridges’’ kutoka upande mmoja wa mtaro hadi mwingine.Katika sehemu kame,cross-ridges zinaweza kusaidia kuhifadhi maji na udongo.Katika maeneo ambayo hayana mvua ya kutosha na ambayo ardhi ni tambarare ama inakaribia kuwa tambarare,mbinu hii huboresha mazao ya mimea.

Upandaji wa mimea inayohimili ukame

Njia moja ya kutumia kwa ukamilifu maji ya mvua ni kupanda mimea inayohitaji maji kidogo.Mimea inayotumiwa wakati wa kiangazi inafaa kuwekwa maanani.Mimea hii huhimili na hukua vyema hata ikiwa mimea mingine itakosa kuzalisha.Inafaa kuwa  mimea ambayo haihitaji maji na mbolea ya ziada ili kumea vizuri.

Mifano hujumuisha nafaka kama mtama badala ya mahindi.hiii ni kwa sababu mtama hutoa mazao mazuri hata kukiwepo na mvua kidogo.Kuna nafaka zingine na mimea ya mizizi na moga ambazo zimepandwa kwa vizazi na zinatoa chakula hata wakati wa ukame.Kuchagua mimea ya kienyeji na aina za hapa nyumbani zinazoweza kupona katika hali ya anga kavu na katika udongo mbovu ni mojawapo wa njia za kutumia kikamilifu maji ya mvua. 

 

0
No votes yet
Your rating: None