Kuna tovuti kadha unaweza pata orodha ya kazi tofauti za hapa nchini Kenya. Wakati unapotuma ombi la kazi kupitia kwa mtandao, unatahadharishwa kwa vile wakora hupenda kuutumia kudanganya watu. Usiitikie kulipa pesa ili uweze kutuma ombi la kazi. Usidhubutu kupatiana mambo ya kibinafsi kama namba ya akaunti ya benki au PINI ya Mpesa. Ifuatayo ni orodha ya tovuti zinazo tangaza kazi za humu nchi na kwengine.
http://www.thesalesjob.com/ - Hii ni tovuti ya Uingereza lakini ina sehemu ya kuchagua nchi mbalimbali na ukichagua Kenya, utapata kazi zilizomo Kenya.
http://www.theitjob.com/ - Hii ni tovuti ya Uingereza lakini ina sehemu ya kuchagua nchi mbalimbali na ukichagua Kenya, utapata kazi zilizomo Kenya.
myjobseye.com - Anayetafuta kazi hujiandikisha na hii kampuni ili waweke wasifu kazi wake kwa orodha ya wanao watafutia kazi. Muajiri akiwa anatafuta mfanyi kazi, atalipa hii kampuni ili impatie majina ya wale waliohitimu kuifanya kazi yake.