Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Andika Wasifukazi (Muhtasari wa maisha yako)

Wasifukazi ni nini?
Ni kibainisho kifupi kuhusu pale umefanya kazi, ulipokwenda shule na maarifa uliyopata. Humpa mwajiri utambuzi wa yale unayoweza kutekeleza na ujuzi ulio nao.

Kwa nini unahitaji wasifukazi?
Madhumuni ya wasifukazi ni kukupa nafasi katika mahojiano. Waajiri huamua ni nani wa kumhoji kulingana au kutegemea na wasifukazi walizopokea kwa kila kazi. Wasifukazi wako unapokuwa maridhawa/bora, una nafasi nzuri ya kuitwa kwa ajili ya mahojiano.

Yanayohusishwa /yaliyomo katika wasifukazi
Ina, anwani, nambari ya rununu pamoja na barua pepe (kama una moja).
Historia ya kikazi (ikihusisha pale ulipofanya, cheo ilichosimamia bila kusahau majukumu uliyokuwa ukiyatekeleza.

Toa habari kuhusu taaluma/elimu/masomo yako.
Taja tuzo/zawadi ama vyeti ulivyopata au kutunukiwa (kwa mfano, “Tuzo ya mwajiri wa mwezi” au tuzo ulizopata shuleni/chuoni).

Maarifa ya kipekee yanayoweza kumvutia mwajiri.
Pata sampuli moja ya wasifukazi ili kukupa mwelekeo.

Jaza Fomu ya Ombi la kazi:
Haya ndiyo yanayostahili kuzingatiwa unapojaza ombi la kazi (Fomu).

Jina lako, Anwani, nambari ya rununu na ya kitambulisho
Majina, Anwani na nambari za rununu za takriban mahali patatu ambapo umefanya kazi, pamoja na tarehe halisi uliyofanya kazi pale.
Jina la mwangalizi/msimamizi wako katika kazi ya awali ama utoe jina na nambari ya mtu kutoka mahali pale anayeweza kurejelewa.

Namna/Jinsi ya kuandika wasifukazi:
Juhudi zako maradufu zitakuelekeza kuandika wasifukazi. Ni kazi rahisi. Pata vidokezi marua vya uandishi wa wasifukazi bora.

Namna/Jinsi ya kutuma wasifukazi:
Unaweza kutuma kupitia posta, kimemeshi/faksi au kumtumia mwajiri wasifukazi wako kupitia baruapepe. Unapotuma wasifukazi, sharti uambatanishe na barua tangulizi (barua ya kuomba kazi).

2.833335
Average: 2.8 (18 votes)
Your rating: None