Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Andika barua ya kuomba kazi

Unapotuma ombi la kazi, unapaswa kutuma barua ya kuomba kazi, pamoja na wasifukazi. Barua ya kazi ni barua anayoandikiwa mwajiri inayoonyesha cheo unachohitaji na kwa nini utakuwa mtu mwema katika kazi hiyo.

Kwa nini unahitaji barua ya kuamba kazi;
Barua hii hukutambulisha kwa mwajiri na inaonyesha maarifa uliyo nayo ama uliyopata ambayo ni ya muhimu kwa mujibu wa kazi uliyoomba.

Jinsi ya kuandika barua ya kuomba kazi:
Shughulikia barua yako kwa mujibu wa kazi unayoomba huku ikionyesha wazi wazi ujuzu na tajriba ya kipekee inayokuwezesha ufae au ustahili katika kazi.

Ifupishe (karibu aya 3-4 fupi, zinazochukua nusu ukurasa)
Jinsi ya kutuma barua ya kazi.

  • Kawaida, tuma barua yako ya kuomba kazi pamoja na wasifukazi.
  • Kupitia kipepesi (faksi): Weka barua yako ya kuomba kazi juu ya wasifukazi.
  • Barua pepe: Tumia barua yako ya kuomba kazi kama sehemu ya barua pepe.
3.153845
Average: 3.2 (13 votes)
Your rating: None