Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Kutoa warejelewa

Warejelewa ni watu wanaoweza kuwasiliana na mwajiri kwa madhumuni ya kujua kama wewe ni mfanyikazi wa aina gani, ni maarifa yepi uliyo nayo na mengine zaidi.

Kwa nini unahitaji warejelewa
Waajiri wengi huhitaji warejelewa ili kupata ithibati ya ujuzi na maarifa uliyopendekeza kwenye wasifukazi. Vile vile, kuhakikisha kama ulitoa habari za ukweli kuhusiana na historia ya kazi kutathmini ni idadi ipi ya watu wanaokujua vizuri na ambao hukuthamini.

Ya kuhusishwa
Orodhesha majina ya warejelewa huku ukitoa anwani zao, nambari ya simu, barua pepe na cheo (kazini au shuleni)

Nani wa kumtumia kama mrejelewa
Watu wanaokufahamu kitaaluma na kibinafsi, msimamizi wa zamani/awali au mfanyikazi mwenza, mwalimu wako wa zamani, posta n.k. Omba ruhusa kabla ya kuwatumia kama warejelewa.

Wakati wa kutoa warejelewa
Kama mwajiri hajaitisha, hamna haja ya kutuma orodha ya warejelewa unapotuma ombi la kazi. Pengine utaulizwa warejelewa wako katika mahojiano. kwa hivyo kuwa na nakala.

4
Average: 4 (1 vote)
Your rating: None