Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Kuingia kazini

Jua jinsi ya kuingia pale: Kabla hujaanza kutenda kazi, fanya jaribio la kukimbia ili kukadiria ni muda gani utakuchukua kufika kazini, halafu ongeza dakika 10 - 15 kwa muda huo kila asubuhi ili kuhakikisha kwamba umewahi kazini mapema.

Fanya maandalizi kabambe: Hujui kitakachotukia kwa hivyo hakikisha kwamba umejiandaa. Uliza jinsi ratiba ya gari la moshi ama basi ilivyo, tengeneza orodha ya watu unaoweza kuwaita kwa usafiri n.k.

Piga simu kama utafika ukichelewa: Kama utachelewa kazini kwa dakika chache, mpigie simu mkubwa/ mwajiri wako ili kumfahamisha kuhusu kuchelewa kwako.

Uliza kama kampuni yako ina mpango wa usafiri: Kampuni nyingine hutoa usafiri kwa waajiriwa wake, hususan wale wanaofanya mpaka jioni au zamu ya usiku. Kampuni yenu pia inaweza kutoa marupurupu ya usafiri. Na kama unataka kutumia gari lako kuelekea kazini, marupurupu ya usafiri hayatozwi ushuru.

Pata msaada wa usafiri kwa wafanyikazi wenza: Uliza kama una mtu katika eneo lenu anayefanya kazi pamoja nawe ili ujiunge katika chama cha kupiga cheki (lift).

0
No votes yet
Your rating: None