Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Ufugaji wa kondoo na mbuzi

Mbuzi na kondoo saa zingine hujulikana kama ng’ombe ya maskini kwa sababu  ya uwezo wao wa kutoa nyama ya kutosha,maziwa,ngozi na ufumwele kwa matumizi ya mkulima na labda masalio kidogo ya kuuzwa.Kuna sababu nyingi kwanini wanyama hawa ni  wa kufaa kuliko ng’ombe kwa mkulima mdogo.

  • Sio ghali kuwanunua(ama kuwa badili) na ni rahisi kuwapata kuliko ng’ombe.
  • Huzalisha mapema,mara kwa mara na wana watoto wengi.
  • Huzalisha kiwango cha wastani cha nyama,maziwa,ngozi na ufumwele kwa matumizi ya familia ama kuuza.
  • Wana uwezo wa kuendelea kuishi kwa lishe yenye ubora wa chini ama katika hali ngumu na kiwango kidogo cha chakula.
  • Huingiliana vizuri na uzalishaji wa mimea na mifugo.
  • Ukubwa wao mdogo unawafanya kuwa rahisi  kwa wanawake na watoto kuwafuga na kuwachunga. 

Wanyama hawa  pia hutoa mfumo mzuri wa akiba na njia  rahisi ya mapato.Mahali ambapo wakulima hawana huduma za benki,mbuzi na kondoo hutoa mfumo mzuri wa uwekezaji  ambao huepuka hatari ya hasara katika uchumi usio imara. 

 

 

0
No votes yet
Your rating: None