Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Ufugaji wa Kuku

Poultry keeping.

Ndege wa kufuga ni kama vile kuku, bata, batamzinga, kanga na bata bukini. Kuku hasa ndio wanaofugwa zaidi na wanapatikana katika boma nyingi nchini Kenya.

Kuku wanaofugwa sana nchini Kenya sio wa ‘gredi’ au wa kuzalisha. Watu wengi hufuga kuku wa kienyeji ambao huachiliwa kuzurura kwa boma wakijitafutia chakula. Hata ingawa kuku wa kienyeji hawatunzwi vizuri, wana thamana kubwa kwa familia nyingi kwa vile mayai na nyama  ni chakula murwa cha protini. Zikiuzwa pia hupatia familia mapato ya pesa.

Shida zinazokumba kuku wa kienyeji zikipunguzwa, wana uwezo wa kutoa mazao ya hali ya juu.

Katika sehemu hii, jifunze jinsi ya kutunza kuku wako vizuri kwa kuwajengea kibanda chenye usalama, kuwalisha vyema na kuwazuia kutokana na magonjwa yanayoathiri kuku. 


 

2.18182
Average: 2.2 (11 votes)
Your rating: None