Kuna njia nzuri na mbaya za kuacha kazi. Kama unaondoka kwa njia nzuri inabidi umtumie msimamizi wako kama mrejelewa. Hapa vipo vigezo vya kuzingatia unapowacha kazi kwa uzuri.
Isetiri mipango yako/Hifadhi mipango yako: Mtu asijue kama unatafuta kazi. Iwapo msimamizi wako au wafanyikazi wenza watajua kuwa utaondoka, kutazuka shida.
Fanya mabadiliko katika wasifukazi: Ongeza kazi mpya ulizofanya katika wasifukazi wako. Pia ongeza majukumu na maarifa mapya uliyopata karibuni n.k.
Endelea kufanya kazi yako vizuri: Njia bora ya kupata kazi ni kuwa na marejeleo mazuri kutoka kwa msimamizi wako wa awali. Ili kutimiza haya sharti uwe na rekodi nzuri ya kazi.
Usisusie kazi iwapo hujapata nyingine: Ni rahisi sana kupata kazi unapokuwa na nyingine unayoshikilia. Salia pale pale mpaka utakapopata kazi nyingine.
Tumia wakati wa likizo yako kufanya mahojiano: Hakuna mtu atakayejua unapoelekea. Lakini lazima utoe habari kwa mwajiri wako kwamba unahitaji muda wa mapumziko.
Pata barua ya udhibitisho kutoka kwa kampuni mpya uliyojiunga nayo: Hakikisha umepata barua inayodhibitisha kwamba unafanya kazi katika kampuni mpya kabla hujaisusia ile ya zamani.
Toa habari ilani toshelezi kabla ya kujiuzulu ilivyo kawaida ni kwamba, inabidi umpe mwajiri wako sasa ilani majuma mawili kabla ya kujiuzulu ingawa kampuni nyingi huuliza na kuhitaji mengi kuhusu kujiuzulu kwako. Tathmini sera za uongozi wa kampuni na uzifuate
Ondoka kwa hali nzuri: Pengine utahitaji kumtumia mwangalizi/msimamizi wako kama mrejelewa wakati wa usoni. Kwa hivyo, hakikisha kuwa hakuna hisia ngumu unapoondoka.