Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Mwongozo wa kuanzisha biashara nchini Kenya

Sewing
Hatua zinazochukuliwa kuandikisha biashara nchini Kenya
  1. Kuchunguza jina: Biashara yako inahitaji jina. Ili usichague jina ambalo linatumiwa na mtu mwingine, lazima uandike barua kwa afisi ya mkuu wa sheria ukipia kitengo cha usajilishaji wa kampuni kuwauliza wakuchunguzie jina unalotaka kuita kampuni yako. Huduma hii hugharimu Ksh. 100 na huchukua siku mbili.
  2. Tengeneza katiba na kanuni za kampuni: Hizi ni stakabadhi za kuonyesha kanuni zitakazofuatwa, mwelekeo na majina ya wale wote wamewekeza katika hiyo kampuni na kiwango cha uwekezaji.
  3. Lipa ushuru wa hati: Pesa utakazolipa hutegemea thamani ya rasilmali uliyotaja. Kwanza lazima uchukuwe fomu nne kutoka kwa shirika la ulipaji ushuru. Kopi mbili utapeleka kwa afisi ya usajili ya  idara ya ardhi, moja unaweka na nyingine unapelekea benki yako.
  4. Jaza fomu ya kuahidi utafuatilia maagizo: Hii fomu hutiwa sahihi na wakili kwa niaba yako.
  5. Kufunguliwa faili ya kampuni: Unapeleka stakabadhi zote za kampuni kwa afisi ya msajili wa kampuni. Hii faili huwa na stakabadhi zifuatazo ambazo lazima uzitafute kwanza:
    1. Tafuta PIN, VAT na PAYE: Hizi ni stakabadhi za ulipaji wa ushuru na zinachukuliwa katika afisi za ulipaji ushuru KRA huko Times Tower Nairobi. Inachukua siku moja kupata stakabadhi hizi zote na hulipishwi chochote.
    2. Sajili Kampuni kwa NHIF: NHIF inasimamia National Hospital Insurance Fund. NHIF ni bima ya afya ya umma.  Hii ni lazima kwa kampuni yote iliyozidisha wafanyi kazi watano. NHIF inapatikana kwa Nyumba ya NHIF iliyo Community hill.
    3. Sajili kampuni kwa NSSF. NSSF inasimamia National Social Security Fund. NSSF ni hazina ya umma ya uzeeni. Ni lazima uchangie hazina hii kwa wafinyikazi wako. NSSF iko katika nyumba ya NSSF katika njia ya Valley Road.
    4. Tafuta leseni ya kufanya bishara jijini: Hii hutolewa na manispaa au baraza la jiji. Kabla hujatuma ombi, lazima uwe na ofifi au mahali pa kufanyia kazi.
7. Tafuta muhuri wa kampuni: Hii ndio sehemu ya mwisho. Kuna mihuri ya kutengenezewa kwa viwanda na ina bei kali. Pia kuna watu hutenegeza mihuri kwa mkono na bei yao ni rahisi.
4
Average: 4 (3 votes)
Your rating: None