Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Jua Mipaka/Viwango Vyako

Kuanza au kuendesha biashara si kwa kila mtu. Unastahili kujiangalia kwa imani na sababu ya kutaka kuendesha biashara yako kabla hujaianza. Je, wewe ni mzuri kutafakari juu ya “Picha Kubwa?” Je, utayamudu makabiliano ya mtu mmoja kwa ajili ya kufaulu au kufeli kwa biashara yako? Je, una ujasiri utakaokuwezesha kuwa muuzaji mtajika wa mawazo yako?

Kuanza biashara mpya au ngeni humaanisha kuwa utatekeleza majukumu mengi. Kwa kiasi fulani hutakuwa na fedha za kutosha kukodisha watu kwa kila kitu, kwa hivyo utamaliza kuwa msahibu, mchoraji, mtawala, fundi, na mengine mengi. Jua mipaka yako. Kama huna ujuzi katika kazi fulani, kama maswala halisi au kuweka hesabu, pata usaidizi. Kama sivyo,utakuwa taabani baadaye na utashusha hadhi kama hufanyi kazi yako vema au kwa wakati unaostahili.

Lazima pia ujue viwango vya maswala ya hesabu. Biashara nyingi imetumbukia katika madeni kwa kuweka matumaini ya kutoa ripoti za hesabu mapema zaidi. Hakikisha una “mpango wa B.” Je,ni yepi yatakayotukia iwapo biashara yako itaanguka kabla ya kupata faida? Je,umekopa pesa nyingi ambazo huwezi kulipa kama hilo linaweza kutukia?

Kama una malipo ya kodi na ya wafanyikazi, hakikisha unalipa kwa kandarasi za muda mrefu. Utakuwa taabani kama utatia sahihi makodisho ya miaka miwili na biashara yako iporomoke kwa kipindi cha miezi sita. Pia, utahitaji bima ya wasio na kazi kugharamia malipo ya waajiriwa utakaoamuru waondoke.
 

0
No votes yet
Your rating: None