Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Kwa nini unahitaji fedha nyingi?

Sio siri. Fedha nyingi huipa biashara yako nafasi nzuri ya kuendelea. Zipo sababu nne za kutaka peasa nyingi ili kuendeleza biashara yako, kuifanya biashara yako kuwa na faida kubwa, na kusaidia biashara yako kuhimili misukosuko.

 • Kuinua biashara yako:
  Unapoanza biashara yako, lazima uwe na pesa za kutosha kwa kipindi cha miezi sita kwa matumizi yako. Ni vizuri kuwa na akiba itakayokuchukua mwaka mmoja hadi mitatu kimatumizi.
 • Kukuza biashara yako:
  Unaweza kutumia pesa taslimu na kuuza vifaa vingi kuafikia mahitaji yako. Pia unaweza kupanua biashara yako kwa kufungua tawi jingine jipya, kuongeza bidhaa au kiwango chako cha uzalishaji.
 • Ili kuifanya biashara yako kuwa na faida kubwa:
  Unaweza kununua vifaa vitakavyopunguza gharama ya uzalishaji au matumizi ya operesheni. Pia unaweza kununua mali kwa wingi kwa misingi ya kipunguzo.
 • Kufanya biashara yako kuhimili misukosuko:
  Unaweza kununua kifaa mapema bila kusubiri mpaka pale malipo yatakapoingia. Unaweza pia kuzuia biashara yako katika hali za chumi zinazosababisha malipo kulipwa pole pole na wateja.
0
No votes yet
Your rating: None