Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Maswala saba unayostahili kufahamu kabla ya kuanza biashara Yako

“Kama nilijua ninachokijua sasa, ningefanya mambo tofauti.”
Je, Unatambuliwa kwa njia zoefu ama iliyozoeleka? Wamiliki wengi wa biashara ndogondogo huyasema haya mara kwa mara. Itazame orodha hii ya maswala ya kuangaziwa kabla ya kuanza biashara.

 1. Uza kile wateja wako wanataka: 
  Usiangazie tu kile unachotaka. Usipotafakari kuhusu wateja wako,kuna uweza wa kutonunua bidhaa yako. Hakikisha unatafiti soko ili kujua kama huduma au bidhaa yako ni ya maana na nafuu kwa uwezo wa wateja.
 2. Andika mpango wa biashara: 
  Hii ni njia moja ya kuwavutia wawekezaji na watoa huduma za kifedha kwa biashara yako. Mpango mzuri wa biashara pia hukusaidia kuweka rekodi zilizo na maelezo zaidi kuhusu ruwaza na malengo yako. Andikda mpango wa biashara.
 3. Uujue uwezo wako: 
  Angazia sana sana yale unayoyafanya vizuri na uwache mengine. Hustahili kujua majibu yote wala kukusanya maswala yote .Kuwa mwaminifu kwa yale unayoweza kutekeleza na yale usiyomudu kutekeleza. Kumbuka, ni vizuri kuomba msaada iwapo hujui kitu Fulani.
 4. Fanya utafiti wako: 
  Tumia madarasa, hafla au semina, vitabu na kanda ili kujifunza yale unayoweza kabla hujaanza biashara.Kama hujui chochote kuhusu uendeshaji wa biashiara, kuna mafunzo mengine ya malipo ya chini, vitabu na kanda.Jaribu maktaba ya mahali pale unapoishi ama hifadhi ya vitabu, na uulize yale yote usiyoyafahamu kuhusu soko, nguvu na uwezo wako, mahali halisi na yale watu wanataka.
 5. Tegemea juhudi zako: 
  Unahitaji kuwa macho katika bajeti yako, la sivyo, utaishia katika madeni makubwa ama utoweke kutoka biasharani haraka sana. Kama huwezi kupata kila kitu unachokiitaji sasa hivi, wachana nacho na ufikirie zaidi kuhusu mpango wako.
 6. Unda mpango wa mauzo: 
  Hili ndilo swala nyeti la kuwavutia wateja wako. Toa ramani ya jinsi ya kupata wateja wa kutumia bidhaa au huduma yako na namna utakavyowasawishi warejee. Unastahili kujiuza ili watu wakujie.
 7. Huwezi kushughulikia biashara peke yako: 
  Unapokuwa na watu wengi wa kukusaidia na vitu “vidogovidogo”,ndivyo utakavyochukua muda mwingi kunawiri biashara yako. Usiogope kuomba usaidizi na ushauri kutoka kwa rafiki zako na hata watu wa familia.
2.10345
Average: 2.1 (29 votes)
Your rating: None