Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Maswali ya kujiuliza kabla ya kuacha kazi yako

Kabla hujaacha kazi yako, jiulize maswali yafuatayo ili kuona kama u tayari kuanza biashara yako mwenyewe.

Je, nina pesa za kutosha za kuanzia (biashara)?
Kama huna pesa za kutosha zitakazokuchukua kwa takriban miezi sita ya kwanza, haupo katika hali nzuri . Unahitaji pesa za mahitaji ya maisha (matumizi ya dharura unapoendelea kusubiri biashara yako ilete faida).

Je, ninaweza kuishi bla malipo imara/murua/mfululizo?
Kama sivyo, haupo tayari.Huennda ikachukua muda mrefu kabla mshahara wako wa kwanza/malipo ya kwanza kuingia.

Je, ninaweza kuanza kuendesha biashara yangu kwa muda mfupi?
Kupitia njia hii, unaweza kuwa na mapato murua, huku ukijenga biashara yako.

Je, nimeandika mpango wa biashara?
Kama huna, andika mmoja sasa hivi.

Je, ninaweza kusubiri kwa miaka 3-5 ili kufaulu?
Hivyo ndivyo inavyokuchukua muda mrefu kuwa mvumilifu.
Je, mimi ni mtaalamu katika nyanja yangu (ya biashara)? Je, ninajulikana katika jamii yangu?

Kama ni hivyo, hii ni sehemu mojawapo ya kukusaidia kuuza mawazo na biashara yako, kusanya pesa/ changa pesa na uwavutie wateja.Kama sivyo, kazi yako itakuwa ngumu zaidi.

Je, nina habari kwamba bidhaa niiuzayo au huduma niitoayo inahitajika katika jamii yangu?

Inabidi ufanye utafiti ili kuhakikisha kwamba wapo watu walio tayari kununua bidhaa ama huduma unazozitoa.

Je, nipo sawa sawa kikamilifu na kompyuta za kutekelezea kazi yangu ya bili, kodi na kuweka rekodi?
Kama haupo sawa, hakikisha una pesa za kutosha kumlipa mtu fulani ukutekelezee kazi hizo.

Je, nina mawasiliano ya kitaalumu ya wafuasi?
Kama ni hivyo, hawa ndio watu utakaotumia kukuenezea habari kuhusu biashara yako na vile vile kusaidia kupata ufadhili, kama sivyo,hii itafanya kazi yako kuwa ngumu.

Je, nina motisha au kuwa mwenye ujasiri, pamoja na ruwaza na uwezo wa kufanya uamuzi?
Kama sivyo, utakuwa na wakati mgumu wa kujenga au kuimarisha biashara peke yako.

1
Average: 1 (1 vote)
Your rating: None