Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Kufanya mambo kwa njia tofauti

Kama unataka biashara yako ya wikendi au siri iwe na mabadiliko makubwa hadi kwa mawazo ya walio wengi unapaswa kufanya mambo yako kwa njia tofauti. Hii inamaanisha nini katika biashara yako? Unastahili kuwa mwangalifu katika sehemu zifuatazo.

Tambulisha biashara yako kwa jina tofouti la kibiashara lililo halisi.

Shirika lolote lenye mwelekeo tawala linalofanya biashara nawe linahitaji uwe halisi. Unahitajika utambuzi halisi mbali na kutambuliwa kwako kibinafsi. Unatakikana kuwa na ushirikiano ulioshikamana/uliofungamana au kuwa na dhima ya ukomo ya ushirika ili kufungua aina nyingine ya biashara. Utahitaji wakili kukusaidia kuyatekeleza haya.

Baada ya kutekeleza ushirika lako halisi, jifaye kwamba serikali inatambua uwepo wako. Hii inamaanisha kwamba wataangalia ripoti za ushuru wa kampuni yako, ripoti za kila mwaka na maswala mengine yatakayokugharimu muda mwingi na pesa.

Hifadhi vitabu vya hesabu na rekodi za biashara yako.
Watu na mashirika ya kibiashara nje ya biashara yako hususan wale wanaokukopa fedha au wale wanaoleta bidhaa, watataka kujua kiasi cha pesa unapata au hasara uliyopata katika miaka iliyopita, raslimali zilizopo katika biashara yako (kama zipo) na malalamishi walio nayo watu wengine dhidi ya raslimali zako.

Lazima uhifadhi vitu na rekodi za biashara mahali tofauti na rekodi za kibinafsi. Maelezo yako ya fedha ya mara kwa mara yanastahili kufanywa ukaguzi na wahasibu waliopendezwa na kuhitimu. Kuhifadhi vitabu na rekodi hizi inaweza kuwa ghali kwa hivyo iinahitaji maarifa ya uhasibu ambayo majasiriamali wengi hawana. Wanastahili kununua huduma hiyo kutoka kwa watu wengine.

Ukaguzi wa hesabu yake utagharimu pesa nyingi sana kutegemea na ukumbwa wa kampuni yako.

Ripoti mapato yako na ulipe ushuru kwa mauzo yako.
Hili linaweza kuwa badiliko kubwa na ghali kwa jasiriamali kuanzia maandalizi ya repoti za ushuru hadi malipo ya ushuru. Makundi ya watu sana sana wawekezaji watahitaji uwape rekodi za repoti za hesabu za miaka mingi ili kukupa mkopo. Wanataka kuhakikisha kwamba mkopo wao umetumiwa kuendesha biashara yako ila sio kulipa ushuru na matumizi mengine.

Pata bima
Haya yanaweza kuwa malipo mazuri. Unaamini kuwa hutaki bima na u tayari kukumbana na hatari? Washiriki wako na wafadhili hawajatulia. Wateja wengi wawekezaji na wasimamizi wao hawataki kufanya biashara na wamiliki wa biashara ndogo ndogo bila aina fulani za bima. Kwa mfano wateja wengi huhitaji wanakandarasi na wachuuzi wao kuwa na bima ambayo inaweza kugharamia majeraha au makosa yoyote yaliyofanyiwa mali yao wakitoa huduma na kuuza kwa niaba ya mmiliki wa mali hiyo.

Kwa njia iyo hiyo kampuni haitakuwa katika hali ya hatari chochote kinapotendeka. Hii ni kweli, wanaotoa mkopo wa pesa hawatatoa pesa kwa biashara bila kutafiti hasa kwa “teleza na anguka” ambapo mtu anaumia kwa ajili ya mali ya aliyekopa.

0
No votes yet
Your rating: None