Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

AFC: Shirika la ufadhili wa kilimo

Hili ni shirika la kifedha linalomilikiwa na serikali na hutoa mikopo kwa mtu ama vikundi vinavyojihusisha katika kilimo ama sekta ya kilimo. Shirika hili lina matawi nchini kote ambako waweza kupata habari kuhusu huduma zao za mikopo na iwapo umehitimu kutuma ombi lako. Hapa ni baadhi ya mikopo ambayo waweza ukapata kutoka kwa AFC:-

  • Mkopo wa mimea ya msimu: Ni kwa wale wanao kuza mahindi na ngano kwa minajili ya kuuza. Mmea wowote ambao hukomaa kwa muda wa miezi kumi na miwili waweza kufadhiliwa.
  • Mikopo ya kununua mashine: Hii ni mikopo inayofadhili mashine zinazotumika shambani kama vile trakta na mashine za kuvuna.
  • Mikopo ya wazalishaji wa samaki: Hii ni mikopo ya ukulima wa samaki, utengenezaji wa bidhaa na biashara inayoambatana na samaki.
  • Mifugo: Hii ni mikopo kwa wafugaji wa ngo’mbe wa maziwa au nyama, ya kuboresha mashamba ya mifugo na pia ukuzaji wa chakula cha mifugo.
  • Mazao ya biashara - Cash Crops: Hii ni mikopo ya upanzi, utunzi, kuvuna na utengenezaji wa mazao ya kibiashara kama vile majani chai, kahawa, miwa, pareto na korosho.
  • Upanzi wa matunda na maua: Hii ni mikopo ya uanziliishi wa biashara na maedeleo ya miundo msingi ili kuboresha ukulima wa matunda na maua.
  • Upanzi wa mimea ya mafuta: Hii ni mikopo ya kukuza mimea inayotoa mafuta kama vile alizeti,  pamba, soya, njugu na mbarika.
3.25
Average: 3.3 (4 votes)
Your rating: None