Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Vyama vya ushirika vya wakulima

Vyama vya ushirika hujumlisha watu wenye nia moja ya kuweka mapato yao pamoja ili watekeleze jukumu fulani ambalo litawafaidi wote. Kuna mamia ya mashirika nchini Kenya na ya wakulima ni mengi pia. Kuna mashirika ya wakulima ambayo yamenawiri na ni kielelezo kizuri kwa wengine.

Mojawapo ya mashirika hayo ni Githunguri Dairy Farmers lililoko Kiambu. Lilianza kama kikundi kidogo cha wakulima wadogo 31 na kwa sasa lina wanachama 12,000, na linamiliki kiwanda cha kutengeneza maziwa  huku likiingiza zaidi ya shilingi bilioni moja kwa mwaka.
 
Ili mashirika ya wakulima yafaulu, ni lazima yajengwe kwa misingi  imara ya kitaaluma, kiufundi na kibiashara. Githunguri Dairy imeweza kufanya hivi kwa kujipanga kwa njia hii:-
 
  • Shughuli za kibiashara na faida ya hayo kwa wanachama: Wametenga maduka ya kuhudumia wanachama ambako wakulima wanaweza kupata vyakula vya mifugo, madawa na huduma za uzalishaji wa ng’ombe(AI) kwa bei iliyopunguzwa. Maduka hayo pia huweka vyakula vya binadamu kama unga, mafuta, mchele, na vyakula vingine ambavyo mkulima anaweza kupata kwa deni kulingana na kiwango chao cha kuleta maziwa. Unatoa stakabadhi yako kisha unapata bidhaa unazotaka. Hii huwapa wakulima motisha ya kuongezea bidii katika kuleta maziwa. 
  • Uboreshaji wa huduma kwa wanachama: Kando na huduma za AI, wanachama wamepangwa kulingana na vitongoji ambako wanapata mafunzo ya ziada kuhusu ukulima. Hii hufanyika kila mwezi na hushughulikia mambo kama uzalishaji, kupata maziwa masafi, mpangilio mzuri wa shamba, biashara ya ukulima, utunzi wa mimea na magonjwa ya wanyama na vile yanavyoweza kuzuiwa. Hii ni kumaanisha kuwa wanachama wana ujuzi wa kutosha na wanapata habari muhimu ya kuboresha ukuzaji wao.
  • Uongozi: Hapa ndipo mashirika mengi yanapofeli. Viongozi hupata vishurutishi vya kisiasa na vya kikabila kutoka kwa wanachama na kupelekea kuwepo kwa migogoro hivyo basi mazao yanabaki kuwa ya chini sana. Kule Githunguri Dairy, nafasi za juu hutangazwa katika vyombo vya habari na kwa sasa mameneja wao ni wataalamu katika mambo ya ukulima wa mifugo na wana shahada za juu na pia sio wazaliwa wa Githunguri.
Fanya mazungumzo na chama chako cha ushirika kuhusu mnavyoweza kuimarisha ukuzaji wenu wa kilimo.  
 

 

0
No votes yet
Your rating: None