Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Bima ya ukulima

Ingawa inawezekana kuichukulia bima biashara yoyote nchini Kenya, wakulima wamepata shida kupata bima itakayoweza kukinga biashara yao dhidi ya hatari wanazokumbana nazo. Wakulima wanakumbana na hatari nyingi kama uharibifu wa mimea kutokana na hali ya anga au wanadamu, maradhi ya mifugo na ya mimea, wizi na uharibifu wa mazao wakati wa usafirishaji hadi kwenye masoko.

Kampuni nyingi za bima zitashughulikia tu mashine kama trakta na mijengo lakini sio mazao. Kampuni moja iliyo na mpango wa bima ya moja kwa moja kwa mkulima ni Blue Shield Insurance. Kampuni ya Blue Shield Insurance  ina bima ya kilimo ambayo hukinga mifugo, mimea na kuku.

Katika mpangilio wa mifugo, bima hii inakinga ng’ombe wa maziwa, ng’ombe wa nyama, mbuzi, kondoo, nguruwe na mamba dhidi ya kifo, wizi na uhamisho. Mpangilio huu waweza ukawa kwa mnyama mmoja kama vile dume ya kuzalisha au zizi nzima.

Mpangilio wa kuku unakinga kuku wa mayai, wa nyama, bata na mbuni dhidi ya ajali, maradhi na wizi.

Mpangilio wa mimea una sehemu mbili ambazo ni kukinga mimea dhidi ya wizi na uharibifu na ya kukinga mimea kama mahindi, ngano, miwa na kahawa dhidi ya uharibifu kutoka kwa moto au radi.

Iwapo uko katika biashara ya ukulima, waweza kuchukua bima ya ukulima ili kuikinga mali katika shamba lako. Tembelea kampuni za bima na uulizie iwapo wana mpango wa bima ambayo inaweza kukufaa kama mkulima.           
0
No votes yet
Your rating: None