Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Chaguo La Kukimu Pesa Zako

Kuna njia aina nyingi za kukimu fedha zako na kulipa bili – kama kadi za mkopo (credit cards), kadi ta ATM, hundi, benki ya intaneti, huduma ya posta au pesa taslim.


Unapotaka kukimu pesa zako, zingatia maswali haya:
 • Una historia ipi katika benki yako? (Una shida kulipa madeni au una rekodi nzuri ya kulipa)
 • Unaweza kutumia pesa ngapi?
 • Je unafuatilia pesa zako vizuri?
 • Ujuzi wako wa hesabati uko vipi?
 • Je mwajiri wako anaweza kutuma hundi ya mshahara moja kwa moja kwa akaunti yako?
 • Kuna benki au mtambo wa ATM karibu?
 • Je unaweza ukatumia mtandao wa intaneti kulipa deni za matumizi yako?

Linganisha aina tofauti za akaunti ili uweze kuchagua inayokufaa.
Akaunti ya hundi (hundi, ATM/Debit Card, kadi ya mkopo (credit card)
Hii akaunti ni ya manufaa na rahisi kutumia lakini ni ghali mno kwa sababu utozaji au malipo yake iko juu. Utatozwa malipo zaidi ukiandika hundi ikiwa hauna pesa za kutosha kwenye akaunti yako. Ni muhimu pia kuhakikisha kwamba umelipia vilivyo matumizi ya kadi yako ya mikopo (credit card) Yafuatayo ni mambo unayopaswa kujua:
 • Lazima ufuatilie matumizi ya pesa zako (kupitia ujuzi wa hesabati au kwa kutizama akauti yako mara kwa mara) ili kuzuia kutoa pesa zaidi kuliko ulizo nazo.
 • Unapotumia kadi ya ATM kutoa pesa, pia tizama baki ya akaunti yako.
 • Unaweza kutumia kadi yako ya ATM/Debit kununua bidhaa au kutoa pesa kwa baadhi ya maduka makubwa kama supamaketi. Kadi hii ni salama kuliko kubeba pesa taslim kwa sababu kadi ikiibiwa au kupotea, unaweza kuzuia pesa zako zisitolewe kwa akaunti.
 • Ukiwa na baki nzuri katika akaunti ya hundi, utapata riba ya juu.
 • Ili uruhusiwe kufungua aina hii ya akaunti, uchunguzi wa hali ya madeni yako unafanywa kuona kama unafaulu.
Akaunti ya Akiba (Na kadi ya kutoa pesa -ATM)

Epukana na hundi zisizofaulu kwa kutumia kadi ya ATM.  Haya ni mambo unayofaa kujua:
 • Akaunti zenye malipo ya chini, kawaida hulipa faida nyingi.
 • Unaweza kutoa pesa na kadi ya ATM na kuangalia baki yako.
 • Unaweza kutumia kadi ya ATM kununua bidhaa na kutoa pesa taslimu hapo kwa hapo katika baadhi ya maduka.
 • Unapotumia kadi ya ATM badala ya hundi, ni vigumu kutoa pesa zaidi ya zilizo katika akaunti yako.
 • Ni vigumu kutoa pesa zaidi ya kiasi kilicho kwa akaunti yako unapotumia kadi ya kutoa pesa badala ya hundi.
 • Ni salama kutumia Kadi ya ATM kwa sababu ikiwa kadi yako imeibiwa au imepotea, unaweza zuia pesa kuchukuliwa kutoka kwa akaunti yako.
 
 
 
 

 

 

0
No votes yet
Your rating: None