Waweza kutumia Benki ya Intaneti?
- Je, umelipa pesa kwa ajili ya kuchelewa kulipa bili?
- Je, umewahi kuchelewa kulipa bili au kusahau kuwa tayari umeshalipa?
- Je, unatumia muda mwingi kuainisha makaratasi ya bili zako?
Kwa nini usijaribu Benki ya Intaneti?
- Mtu wa kawaida akitumia benki ya Intaneti anachukua dakika 15 kwa mwezi kulipa bili badala ya saa tatu au nne.
- Wizi wa nakala zilizo na mambo ya kibinafsi kama vile Pini ya ATM na kadhalika hutokea kupitia wizi wa vibeti au vitabu vya cheki na sio hutufunza kompyuta.
- Mamilioni ya watu hutumia benki ya Intaneti.
Ni rahisi na salama kutumia benki ya Intaneti. Hata hivyo, kuna vitu vidogo vidogo unavyostahili kujua kabla ya kuanza kutumia benki ya intaneti.