Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Kabla hujaweka tangazo

Jiulize na uyajibu maswali yafuatayo kabla hujaanza kampeni za matangazo yako.

 • Je nipo tayari “kufikia” wateja wangu kwa takribani mara sita?
  Mteja wa kati huhitaji “kufikiwa mara sita kwa njia ya matangazo na vijibarua vya matangazo ama vyombo vingine vya mauzo vilivyo na toleo la biashara.
  Kununua/kulipa tangazo moja kwenye magazeti ya humu nchini si muhimu. Panga njia karibu sita utakazotumia kuifikia hadhira yako.
 • Nataka kufikia nini?
  Jua wazi walio wateja wako na pale walipo. Tambua wanachokisoma, wanachokisikiliza na kutazama ili kujua njia nzuri ya kuwafikia.
 • Lazima ninunue/nilipie tangazo kwenye magazeti, majarida, redio au televisheni?
  Bajeti itawajibikia chombo cha habari unachochagua. Kitengo cha uandishi/ magazeti na televisheni vyote vitafaa. Matangazo kwenye redio huwa ghali, lakini hata hivyo, unaweza kutumia redio ya kienyeji.
  Onyesha tangazo lako kwenye sehemu mwafaka ya magazeti na majarida. Angalia uone kama magazeti yanaonyesha sehemu fulani za arusi, Siku kuu, kurudi shuleni, kustaafu, mipango na mengine mengi. Wasomaji huweka sehemu hizi; kuwa hizi ndizo sehemu nzuri za matangazo.
  Kwenye matangazo ya redio au televisheni, chagua programu/vipindi vinavyopendwa na wasikilizaji na watazamaji.
 • Nafasi iliyobaki ni ipi?
  Magazeti huwa na nafasi zilizobaki mara nyingi kwa kusudi la kipunguzo wakati wa uchapishaji kama hawajaanza sehemu fulani za kurasa zao. Hakikisha una kamera tayari kwenye hali kama hizi za dakika za mwisho mwisho.
 • Ni kipi ninachokihitaji mteja afanye?
  Kila tangazo lazima liwe na njia ya mawasiliano ili kufikiwa rahisi na wateja wako, wakuite ama wafungue/waiangalie tovuti yako. Tambua lengo la tangazo lako kabla hujalilipia.
 • Ni jinsi gani nitafuata matokeo?
  Ni kufuja/kupoteza pesa katika matangazo iwapo hujui kama tangazo hilo limetekelezwa kuwa na mfumo wa kufuatilia. Waulize watu namna walivyosikia kukuhusu wewe au waulize warejelee tangazo lenyewe iwapo watawasiliana nawe.

 

0
No votes yet
Your rating: None