Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Kufanya mauzo kwa kutumia neno la kinywa/mdomo

Biashara ifanywayo kwa kuelekezwa si ghali, ni njia mwafaka ya kuleta wateja wengi. Pia ni bora na chombo rahisi cha mauzo kilichopo. Hapa kuna maswala ya kuongeza biashara unayopata kwa kuelekezewa wateja.

  • Fanya kazi nzuri na wateja wako waliopo. Ni jukumu lako kuwa na ujuzi upendezao kwa wateja wako. Wape huduma bora na yenye thamani kubwa.
  • Pata majibu ya wateja wako kila wakati. Waulize kama wanaifurahikia kampuni yako na huduma waipatayo. Kama unasikia kauli yoyote ya namna ya kuendelea vizuri, jibu haraka. Wateja wataonekana wenye kushukuru na wenye thamani kubwa unapowasikiliza.
  • Watuze wateja wanaokuelekezea wateja wengine katika biashara yako. Kinyozi au msusi anaweza kutoa tuzo 10 kwa wateja wengine walioelekezwa kwake bila kuwasahau wale waliowaelekeza. Mteja mgeni anafurahi na Yule, sasa unatambuliwa kutokana na juhudi zake.
  • Shirikiana na biashara nyingine ujiranini mwako. Anayetoa mafunzo ya mazoezi ya mwili anaweza kutoa hati ya pesa kwa duka la vyakula vya afya huku duka hilo likitoa tarahani (kipunguzo) cha asilimia kumi (10%) ya hati pesa ya wanachama kwa mkufunzi huyo wa mazoezi. Biashara zote hufaulu.
  • Wasiliana katika miungano ya biashara pale ulipo. Baraza la biashara na mashirika mengine ni mahali pazuri pa kuwajua watu kwa kufanya miungano ya kipekee na kitaalamu.
  • Zungumza kila mara na wateja wako. Tumia postikadi, majarida au vidokezo vya barua pepe. Wahimize wateja wako waelekeze biashara yako kwa rafiki zao na familia. Dobi anaweza kutumia vidokezo vya msimu kuhusu jinsi ya kuhifadhi nguo, uhifadhi mzuri wa sweta katika msimu wa vuli(mvua nyingi) na namna ya kuzifanya nguo zako zidumu kwa muda mrefu. Jumuisha hati mbili za pesa, moja ya mteja na nyingine kwa rafiki au mtu wa familia.
0
No votes yet
Your rating: None