Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Wawekezaji

Pata pesa kutoka kwa Private Equity Funds (PEFs) au Venture Capitalists
PEFs na VCs ni kampuni za michango ya uwekezaji na huwa wana kiwango kikubwa cha fedha. Kwa kawaida huwekeza kiasi kikubwa cha fedha. Wakiwekeza katika kampuni, wanamiliki sehemu moja ya na hushughulika na mwongozo na usimamizi wa kampuni. Ni ngumu sana kuwapata wawekezaji hawa – kawaida hupendelea kuwekeza katika kampuni zilizo na uwezo wa kufanikiwa na kutengeneza faida ya mamilioni baadaye.

Pata pesa kutoka kwa wawekezaji ‘malaika’
Wawekezaji malaika (watu binafsi au makampuni) hutafuta biashara zilizo na umahiri na uwezekano wa kutengeneza faida.

Pata pesa kutoka kwa mipango ya kutia motisha kampuni mpya (Industry Incentive Schemes)
Viwanda vingi vya uzalishaji hutoa mchango kwa kampuni mpya zinazotumia au kuuza bidhaa zao ili kuwapa motisha wa kuendeleza biashara.

Pata pesa kutoka kwa wafadhili.

Pata pesa kwa kuuza sehemu ya kampuni yako kwa soko la hisa.
Kutoa na kuuza hisa za kampuni yako kwa raia kunajulikana kama ‘kwenda hadharani’. Yeyote anaweza kumiliki sehemu ya kampuni yako. Kwenda hadharani kunaweza kukuletea pesa nyingi lakini kampuni nyingi hazipendelei ‘kwenda hadharani.’

0
No votes yet
Your rating: None