Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Hali ya anga na usimamizi wa ardhi na maji

Maharagwe ya kawaida hukua kwa kipimo cha joto la nyuzi 17.5 hadi 27. hali ya kiwango cha juu cha joto zaidi ya nyuzi 30 yaweza kufanya mbegu ambazo bado no changa na kwa joto zaidi ya nyuzi 35 huenda mbegu zisikomae. Maharagwe ya kawaida haswa hukuzwa kwa urefu wa vipimo vya mita 600 hadi 1950.

Maharagwe yanahitaji mvua ya kadri ya kati ya milimita 300-400 kwa upanzi mmoja wa mimea ingawa ali ya anga isiyo na mvua wakati wa kuvuna pia inahitajika. Hali ya kutokuwa na mvua kwa muda mrefu ama kuwepo kwa mvua kupita kiasi huharibu mazao ya maharagwe. Maharagwe yanayomea kwa kuegemea kwa mimea mingine hufanya vyema katika sehemu zilizo na mvua nyingi ilhali aina ya ‘dwarf’ huwa na mazao mabovu ikiwa mchanga una unyevu mwingi. Aina ya udondo unaotoa mazao mengi ni ule mwepesi ama ulio mzito kadri na pia ulio na mbolea na kiwango cha chini sana cha mchanganyiko wa madini (chumvi na sukari)-(PH) na usishikilia maji mengi sana kwa muda mrefu. Maharagwe ya kawaida huhitilafiana sana na chumvi.

Kiwango cha nyuzijoto ambacho no mwafaka kwa ukuzaji wa maharagwe ya asili ya kifaransa ni 20 hadi 25 ingawa pia yaweza kuzwa katika nyuzijoto kati ya 14-32. joto lililopita kiwango hupelekea kuwepo kwa mimea mibovu. Hata hivyo. Maharagwe haya hukomaa kwa haraka kwenye sehemu zilizo na joto. Maharagwe haya yaweza yakakuzwa kwa urefu wa kati ya mita 1000 hadi 2100.

Ukulima unaopata maji ya mvua wawezekana katika sehemu ambazo zina mvua iliyosambaa vyema, iliyo kadri na ya kiwango cha juu cha kati ya milimita 900 hadi 1200 ingawa kuhakikisha kuwa kuna mazao bila kukoma haswa sana wakati wa kiangazi unyunyuziaji wa maji ni muhimu. Wakati wa kiangazi, maji ya kiwango cha hadi milimita 50 kwa wiki kinahitajika. Hii inaweza kufanyika kupitia kwa unyunyuzaji kwa njia ya mitaro ama kutumia mifereji hewani. Maharagwe ya asili ya kifaransa humea vyema zaidi katika mchanga usioshikilia mji mengi, mchanga ulio mwororo na ulio na mbolea ya kiwango cha juu(pH) kama 5.5 hadi 6.5.

2
Average: 2 (1 vote)
Your rating: None