Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Uzalishaji na upanzi

Uzalishaji wa kawaida ni kwa njia ya mbegu lakini kwa madhumuni spesheli sehemu ya kijiti ya mmea hutumika. Kwa maharagwe ya kifaransa ambayo hukuzwa kwa malisho ya mara moja, upanzi hufanyika kwa nafasi ya majuma mawili hadi matatu ndiposa kuwe na mavuno mwaka mzima ingawa wakati mkubwa wa kuyauza maharagwe haya katika soko la ngambo ni Oktoba hadi Mei.

Ili kuzuia wadudu na maradhi ni sharti uepuke kupanda maharagwe kwa karibu sana. Humu nchini Kenya, nafasi ya kati ya sentimita 30x15 kwenty mitaro ya upanzi inapendekezwa. Upanzi mpya ni vyema ufanyike sehemu za mbele ambako hakujapandwa na ambako upanzi wa mfululizo unafanyika. Panda mahindi, nafaka au ‘sunflower’ katikati ya maharagwe ya kifaransa ili kudhibiti kuenea kwa magonjwa yanayosababishwa na upepo kaka vile ‘bean rust’.

Wingi wa mimea ni 150,000-200,000 kwa ekarimoja kwa ile mimea isiyokuwa mirefu na nusu ya hiyo kwa ilew inayokuwa na kimo kirefu kwa upanzi wa mmmea mmoja. Katika upanziwa mchanganyiko ule wingi wa mimea uko chini kiasi. Kwa maharagwe yaliyo na urefu wa kimo kikubwa, mbegu 4 hadi 6 hupandwa pamoja kwenye vilima vilivyo tofauti na kwa mita moja. Pia yaweza kupandwa kwa mitaro ya nafasi ya sentimita 90-120x15-30. Vina vya mashimo ni sentimita 3 hadi 6. Wingi wa mbegu utakazopanda unalingana na ukubwa wa mbegu na na wingi wa mazao unayotarajiahii ikiwa ni kilo 120 kwa ekari moja kwa maharagwe ya kimo kidogo na kilo 60 kwa maharagwe ya kimo kirefu kwa ukulima wa mmea mmoja. Mimea inayojishikilia inapomea huhitaji kushikiliwa na vijiti vya hadi mita 2.5 kwa urefu labda kama impepandwa na mimea mingine mirefu kama mahindi ama mtama, hali ambayo imechukuliwa na wakulima wengi mkoani Rift Valley ambapo mahindi ama mtama hutekeleza wajibu wa kuwa kigongo cha kushilia mimea.

Jizuie na upanzi wa maharagwe karibu na kunde, soyabeans na mimea mingine ya sampuli hiyo ambayo yaweza kuwa chanzo cha nzi wa maharagwe yaani bean flies.

Jizuie dhidi ya kupanda maharagwe karibu na kunde, soya na mimea mingine ya aina hii ambayo huenda ikawa ndio chanzo cha nzi wa maharagwe-bean flies.

Aina za maharagwe ya asili ya kifaransa zinazopatikana kwa wingi nchini kenya
 

Variety Resistance to diseases
Amy Anthracnose / Common bean mosaic virus
Emelia Anthracnose / Common bean mosaic virus / Halo blight
Julia Anthracnose / Common bean mosaic virus
Lausanne Anthracnose / Common bean mosaic virus
Paulista Anthracnose / Common bean mosaic virus / Common blight
Olivia Common bean mosaic virus
RS 1389 Common bean mosaic virus / Bean rust
RS 1391 Common bean mosaic virus / Bean rust
RS 1518 Anthracnose / Common bean mosaic virus
Samantha Anthracnose / Common bean mosaic virus
Tanya Anthracnose / Common bean mosaic virus / Halo blight
Xera Anthracnose / Common bean mosaic virus

 

Source: PIP Technical Itinerary French Beans. www.coleacp.org/pip

0
No votes yet
Your rating: None