Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Utumizi wa mbolea

Maharagwe ni amimea ambayo hutumia kiwango kidogo cha mbolea na huhitaji kama kilogramu 25-35 kwa ekari moja(hii ni sawa na mfuko mmoja ama miwili ya mbolea aina ya mijingu rock phosphate na kilo 75 hadi 80 za kilo kwa ekari moja. Kama mimea mingine ya sampuli yake, maharagwe yanao uwezo wa kutia madini ya nitrogen kwenye udongo kutoka angani kwa hivyo hayahitaji mbolea ya nitrogen. Hata hivyo udongo unaokubali madini ya nitrogen kutoka kwa chembe chembe za kiasili zilizo na madini hayo ndio unaokubalika kwa haraka.

Udongo mgumu ulio na mbolea ya kiasili ya kiasi kidogo haupeani mazao mazuri ya maharagwe hadi mbolea ipeanwe kwa njia ya taka ama samadi iliyooza na kuwa mbolea laini. Ili uwe na maharagwe yanayomea wima na bora kujenga ‘nasari’ za upana wa hadi mita 1 ili kuzuia kujaa kwa machanga kando kando mwa mimea. Uwekaji wa mbolea iliyo nzuri kwa hiyo mimea utahakikisha mazao yameimarika kwa kuwa itasaidia katika uwekaji wa madini ya nitrogen mchangani.

Kupalilia kwa wakati na kuliko shawri kunuhitajika kwa maharagwe ya asil ya kifaransa. Kupalilia kwa kwanza ni sharti kufanyike majuma 2 au 3 baada ya kuchipuka kisha kupalilia kwa pili kufanyike majuma 2 hadi 3 baadaye. Wakati wa kupalilia, kutengeneza vijitaro vidogo kwaweza kusaidia maharagwe kustahimili athari za nzi wa maharagwe. Kupalilia maharagwe mchanga ukiwa na maji kwaweza kupelekea kusambaa kwa maradhi yanayotokana na udongo kama vile ‘anthracnose na furasium root rot.’

Kupalilia kwa juu juu kunahimizwa haswa kwa wakati kabla ya kutoa ua kwani kuharibika kwa mizizi ya mimea kunaweza kukaleta maradhi ya udongo. Maharagwe ya kawaida yanaweza kunyunyuziwa maji au yaka tegemea maji ya mvua. Unyunyuzaji wa maji ni wa maana katika sehemu zilizo na ukame huku kunynyuzia kwa njia ya mifereji ya juu kukiaminika zaida ya unynyu zaji unaokaa ni kama eneo limefurika. Kwa ukulima wa wenye mapato ya chini ni nadra mimea ipate mbolea. Upanzi wa mimea tofauti wakati tofauti ni muhimu ili kudhibiti magonjwa kama vile ‘bean rust, powdery mildew. Anthracnose na fusarium root rot.’

Weka mbolea inavyohitajika kisha upande maharagwe ya asili ya kifaransa kwenye vilima ambapo gonjwa la ‘root rot, huenda likawa ndilo tatizo. Epuka unyunyuzaji wa maji kupitia kwa njia ya mitaro kwenye sehemu zilizo na maradhi ya ‘root rot’ na wadudu waitwao root-knot nematodes.

Kunyunyuzia nyasi na matawi juu ya mimea
Hali hii inasaidia kuhifadhi unyevu, kumea kwa mizizi inayosaidia kudhibiti mimea na huongeza udhibiti dhidi ya uharibifu wa nzi wa maharagwe.

 

Upanzi wa mimea tofauti katika sehemu moja
Maharagwe hufanya vyema yakipandwa na mimea mingine kama mahindi, viazi na biringanya na yaweza kuongezea madini ya nitrogen kwa hiyo mimea mingine ingawa kwa kiwango fulani tu. Upanzi wa maharagwe kwa muda mrefu kwaweza kuongezea madini ya nitrogen kwa kiwangi kikubwa kushinda upanzi wa muda mfupi. Kuyapanda maharagwe pamoja na chives or garlic husaidia kuzuia wadudu aina ya ‘aphids’

Usimamizi wa maji
Kuwepo kwa maji wakati wowote yanapohitajika ni muhimu kwa maharagwe ya kifaransa kwani unyevu huathiri mazao, usawa wa kukua kwa mimea na kiwango cha mimea. Ukosefu wa maji wakati mimea inapimea maua huathiri mazao kama vile maji mengi zaidi hufanya. Unyunyuzaji wakati wa kiangazi unahimizwa kama vile mvua ya milimita 35 kwa wiki wakati wa upanzi na siku kumi baada ya kuchipuka kwa mimea, kufuatiwa baadaye na milimita 50 kila juma hadi kukomaa.

Kuzuia kwa wadudu ma maradhi kwa kutumia EM ama BM
EM na BM ( effective microorganisms and bioactive microorganisms) zimeonyeshwa kuwa zenye uwezo wa kuzuia maradhi mengi na wadudu kadhaa kwa mimea inponyunyuziwa mara kwa mara. Zinapatikana madukani na pia si za bei ghali mno.

0
No votes yet
Your rating: None