Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Hali ya anga, mchanga na usimamizi wa maji

Kunde hutoa mazao mazuri zaidi na ya hali ya juu katika mandhari isiyo ya jua kali na yenye unyevu. Mimea hii hukuzwa vyema zaidi kati ya nyuzi 10 na 30 kiwango kilicho bora zaidi kikiwa nyuzi 20. Hali ya joto zaidi ya nyuzi 30 yaweza kusababisha kuokmaa kwa mapema na mazao machache. Unyevu wa kiwango kilicho sawa ni hitaji la kunde, haswa wakati wa kumea ua na kukomaa kwa mbegu. Kiwango cha chini cha mvua cha kama nyuzi 400 hadi 500 kwa msimu mmoja wa upanzi( kama miezi mitatu) kinahitajika kwa ukuzaji wa kunde bila kunyunyuzia maji. Katika maeneo yaliyo juu, zao hili lazima likuzwe kwa urefu wa zaidi ya mita 750. Kunde zaweza kukuzwa kwa aina nyingi za udongo ingawa hukuwa vyema zaidi katika udongo usioshiklia maji mengi na ulio na pH of 6 to 7.7 na ulio na kiwango kikubwa cha mbolea. Wakati wa kupanda na mahali pa kupanda mimea tofauti katika misimu tofauti(crop rotation) hutegemea na hali ya anga ya eneo hilo, mchanganyiko na lengo la kukuza, iwapo ni ya kupelekwa ng’ambo ama ni ya matumizi ya humu nchini. 

0
No votes yet
Your rating: None