Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Uzalishaji na upanzi

Kunde hupandwa mara moja kwenye mchanga uliotayarishwa vyema na ulio na unyevu. Mbegu za kunde sharti zipandwe katika shimo la kina cha sentimita 2.5 iwapo huo mchanga una kina kirefu. Kwa mchanga uliokauka na ulio mwepesi mbegu sharti zipandwe kwa vina vya sentimita nne. Mimea ya kunde inahitaji mchanga ulio na joto kiasi ili ikue vyema na nafsi inayotosha ili ipate jua. Mbegu lazima zipandwe kwa vijitaro vya kimo cha sentimita 10x50 hadi 60. Iwapo mgawanyo ushafanywa, hili hutendeka katikati ya vijitaro viwili kwa kutumia vijiti ama nyaya fupi na nyuzi.

Kwa udongo ulio na mbolea ya kiasi cha chini, kiasi cha hadi tani 20 kwa ekari za mbolea sharti zinyunyuziwe kabla ya upanzi na pia hadi kilo 200 za madini ya ‘rock phosphate’ kwa ekari. Kwa vile kunde ina madini ya ‘nitrogen’, basi mbolea ya madini hayo haina manufaa yoyote ya ziada kwa mimea hii, hata hivyo inahimizwa kuwa mbegu hizo zipandwe na madini ya ‘rhizobium’ ili mimea hiyo iweze kuweka madini ya kutosha ya nitrogen kwenye mchanga kutoka hewani. Kuongezea madini ya ‘rhizobium’ kumeonyesha kuongeza mazao kwa asilimia 100. Unahimizwa kuchanganya mimea ilyotupwa na mbolea iliyooza kwa kimo cha sentimita 20 kwenye mchanga kabla ya upanzi. Hii huharibu magugu yaliyo shambani na kupelekea kuwepo kwa ardhi nzuri ya kupanda mbegu.

 

0
No votes yet
Your rating: None