Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Kuvuna

Kunde huwa tayari kwa kuvuna majuma 8 hadi 12 baada ya kupanda. Wakati wa kuvuna utaamiliwa na kuonekana kwa maganda. Kwa kunde aina ya garden peas hii ni kumaanisha maganda lazima yawe.

Yamejaa vizuri na pia ni laini nab ado ni kijani kibichi. Kunde ya maganda huvunwa punde mimea hiyo inapokuwa kubwa lakini kabla ya mbegu kujiunda. Vile maganda yanavyokomaa ndivyo sukari iliyomo katika mimea inavyozidi kupunguka huku bei yake ya soko ikidorora. Msimu wa kuvuna hukaa kwa muda wa majuma 4 hadi 6. Mavuno hutofautiana kutoka tani 1.5 hadi tani 5 za mbegu zilizo kwenye maganda kwa ekari ikiwa mavuno yenyewe ni ya takriban tani 2.5 hadi 3.5 kwa ekari. Kwa soko jipya, zao la kunde hutofautiana kutoka tani 3 hadi 10 kwa ekari au takriba tani 5 hadi 6 kwa ekari. Kundi inayolika na iliyo kwenye maganda kwa kawaida hutoa tani kuanzia 3 hadi 5 kwa ekari. Kwa soko jipya liwe ni la huma nchini ama la ng’ambo, mimea ilivunwa huchujwa na kupakiwa. Kuosha hakuhitajiki kwa vile kunaweza kuharibu kunde hivyo basi mbegu zilizoshika mchanga hutupwa pamoja na mbegu zilizomea vibaya au zilizo na magonjwa. Kunde iliyokataliwa huwa lishe bora kwa wanyama.

Kwa kunde iliyokauka, mmea wote waweza ukang’olewa iwapo asilimia 80 ya maganda imekauka na kubadilika kuwarangi ya maji ya kunde. Mazao hayo aidha yatawachwa shambani ama yabebwe hadi sehemu nyingine ambapo yatakauka kabisa kasha yatagongwa kuchaguliwa.

 

0
No votes yet
Your rating: None