Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Hali ya hewa, ardhi na usimamizi wa maji

Mimea ya soya hukuzwa sehemu za Equator hadi digri 55 kaskazini ama digri 55 kusini na kimo cha mita 2000 kuanzia chini ya bahari. Iwapo ni zaidi ya mita 2000 zile aina zinazochukua muda kukomaa huchukua hadi siku 180(miezi sita) ingawa hutoa mazao mengi kuliko zile aina ambazo hukoma kwa haraka. Soya hukua wakati jua linapowaka. Nchini Kenya, soya hukuzwa katika maeneo ambayo hupanda mahindi haswa sana na wakulima wadogo. Joto chini ya nyuzi 21 na zaidi ya nyuzi 32 linaweza kuwa kizingiti kwa kumea kwa soya ma kuundika kwa maganda.

Iwapo kuna maji, soya yaweza kukuzwa mwaka mzima katika maeneo ya tropic na sub tropic. Soya inahitaji kati ya milimita 400 hadi 500 kwa msimu mmoja kwa mazao mazuri. Unyevu mwingi unahitajika wakati wa kuchipika kwa mimea hii, kutoa ua na kujiunda kwa maganda. Hata hivyo ukosefu wa mvua unahitajika wakati wa kukomaa. Wingi wa mvua kwa muda waweza ukastahimiliwa na soya lakini kuharibika kwa mbegu ni shida kuu wakati wa mvua.

0
No votes yet
Your rating: None