Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Uzalishaji na upanzi

Soya huzalisha kutumia mbegu. Hata hivyo mbegu ya soya yaweza ikapoteza huo uwezo kwa kti ya miezi 6 hadi 10 kulingana na aina yake na mazingara haswa mahali palipo na joto jingi au unyevu mwingi. Jaribu iwapo mbegu ilizonazo zinaweza kumea kabla ya kupanda: chukua mbegu mia moja kutoka sehemu tatu tofauti katika mkoba wako wa mbegu kasha uweke kila mbegu kwenye glasi ya maji kwa masaa 24, yamwage maji halafu utie pamba ilyo na maji ama nguo iliyo na maji. Nguo hiyo ibaki na unyevu, baada ya siku tatu ama nne mimea itaanza kuchipuka kwa mbegu zilizosawa, na itakuwa rahisi kuhesabu ni ngapi kati hiyo mia moja itakuwa imemea (asilimia ya kumea). Soya pia yaweza kupandwa katika mashamba ya mpunga. Katika mashamba ya mpunga, soya hupandwa bila kulima baada ya kila msimu wa kuvuna kufuata mistari iliyoachana na ukubwa wa sentimita 25x25x20. Katika mashamba yaliyolimwa soya hupandwa katika mistari iliyoachana kwa sentimita 40-50 na ndani ya kila mstari mbegu hupandwa zikiachana kwa sentimita 10. Mbegu hupandwa kwa kiwango cha kilo 60-70 kwa ekari. Kupanda kwa kurusha punde tu baada ya mpunga kuvunwa pia kunafanyika.

Aina za Soya zinazohitajika kukuzwa katika sehemu tofauti nchini

 

Maelezo Sehemu nchini kenya Aina

Sehemu zina joto
Homa Bay "Duicker," "EAI 3600," "Nyala"
Sehemu zilizo na joto ya wastani Bukura, Kakamega, Manor House, Embu "SCS I," "Duicker," "Nyala," "Gazelle"
Sehemu zilizo na baridi Bahati, Baraton, LH2, Menengai "Sable," "SCS I," "Nyala," "Gazelle"
Kusipo na mvua nyingi Matayos, Gachoka, Makueni, Ol Rongai "Gazelle," "EAI 3600," "Nyala," "Sable"

 

0
No votes yet
Your rating: None