Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Kuvuna

Aina zinazokomaa kwa haraka zaweza kuvunwa siku 70 baada ya upanzi ilhali zinazokomaa kwa kukawia huhitaji hadi siku 180. Mimea yenyewe hukatwa karibu na udongo ama kuvutwa na mizizi yao inapokomaa wakati ambapo matawi mengi yamebadili rangi hadi hudhurungi na ganda moja hivi kwa kila mmea limebadili rangi hadi maji ya kunde ua nyeusi. Soya za mboga huvunwa maganda yakiwa bado kijani kibichi lakini kama mbegu zimeshjaza maganda yenyewe. Wakulima wengi wa kiwango kidogo hupata mazao ya kiwango cha kilo 500 hadi 1000 kwa ekari ingawa kilo 3000 zinawezekana iwapo kuna utunzi mzuri wa mimea na aina zilizopigiwa upato.

Soya inaweza kuvunwa kwa mikono ama kwa mashine aina ya combine harvester (hii ni baada ya kukomaa ama baada ya kukata mimea hiyo na kuiwacha kwenye jua ili ikauke vizuri). Baada ya kugonga, kausha soya hadi kiwango cha unyevu kiwe chini ya asilimia 12 kabla ya kuhifadhi. Hifadhi katika chumba kilicho kisafi na uwazuie viwavi kwa mbinu yoyote kati ya zile ulizoorodheshewa kwa wadudu wanaoshambulia mazao yaliyohifadhiwa. Mbegu zilizowekwa kwa minajili ya upanzi hazitakikani ziwekwe kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa vile zitapoteza uwezo wa kumea.

 

0
No votes yet
Your rating: None