Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Upanzi wa zaidi ya aina moja ya mmea

Ukulima wa soya hufanyika kama wa mmea mmoja ama pamoja na mimea mingine kama mahindi, mihogo, mtama, ndizi, miwa, mnazi na miti ya matunda. Kati ya mahindi na mtama, soya yaweza kupandwa katikati ya mistari miwili. Kupanda soya na mahindi huleta wadudu ambao huzuia kuenea kwa vijidudu viitwavyo African bollworm na pia hutumika kama kizingiti kwa magugu. Soya haitakikani kukuzwa mahali pamoja kwa zaidi ya miaka miwili ili kuzuia kuchipuka kwa magonjwa yanayotokana na udongo. Panda kwa kubadilisha mimea kwa miaka mitatu ama minne kama njia ya kudhibiti maradhi. Soya hukuwa vyema zaidi ikipandwa punde tu baada ya kuvuna mahindi lakini haipaswi kupandwa baada ya maharagwe ama sunflower kwa vile maradhi ya white mould yanaweza kusambaa.

Udhibiti wa magugu ni muhimu. Utayarishaji wa mapema wa shamba na kungoa nyasi ndicho kipengele cha kwanza unapotaka mazao mazuri. Unyunyuziaji kwa wingi unahitajika kwa mchanga usioshika maji na sio mzito kama ule wa mfinyanzi. Soya husaidia katika kulainisha udongo na pia rutuba kwa sababu ya uwezo wa kuweka madini ya nitrogen kwenye mchanga. Soya hupata mahitaji yote ya nitrogen kutoka hewani wakati ambapo bacteria aina ya rhibozia ipo mchangani. Kuingia kwa madini ya nitrogen ni kwa sababu ya uhusiano baina ya bacteria ya rhizoba na mimea hiyo. Iwapo soya haijapandwa hapo awali, ni vyema kutibu mbegu zako na ‘soyabean inoculum(rhizobium japonicum) ambayo inapatikana katika chuo kikuu cha Nairobi-Kabete, kitengo cha sayansi ya mchanga kwa kiwango cha gramu 100 kwa kilo 15 za mbegu kabla ya upanzi ili kuwepo na kuingia kwa madini ya nitrogen msimu wote. Mmea ulio na vizizi inavyostahili huwa na vijizizi 5 hadi 7 kwa mzizi wake. Wakati ambapo mimea ina vijizizi (nodules) vichache, chunguza kwa makini kujua iwapo vitaongezeka. Ukosefu wa nitrogen hupelekea kuwepo kwa matawi yasiyo na rangi inayostahili. Usiongeze madini ya nitrogen kwa soya ilyo na vijizizi vya kutosha. Hiyo ni kuharibu muda na fedha. Nitrogen ikiongezwa wakati wa upanzi hufanya kumea kwa vijizizi kuchukue muda. Hata hivyo madini ya phosphorous iliyo katika maumbo ya rock phospahate kwa mgao wa kilo 100 hadi 150 kwa ekari moja ni ya faida sana kwa kumea kwa mizizi.

0
No votes yet
Your rating: None