Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Jinsi ya Kuanza Kuweka Akiba

 

 Ikiwa ungetaka kuanza kuweka akiba, yafuatayo ni mashauri sita ya jinsi utakavyoanza. 

  1. Weka Lengo: Ukitaka kufaulu, lazima uwe una kitu unalenga kununua. Fikiria itakugharimu pesa ngapi kununua kitu hicho?
  2. Jilipe kwanza: Ukipata mapato yako, kabla hujatumia pesa zozote, weka kando kiasi fulani kila mwezi. Dhania kama unajilipa.
  3. Unda bajeti: Nakili mpango wako wa matumizi. Utahitaji mwongozo wa jinsi ungetaka kutumia pesa zako.
  4. Fuatilia matumizi yako: Hiki ni kitengo cha pili cha bajeti yako. Haitoshi kuandika malengo yako. Hakikisha unayafuatilia. Ukiweka risiti na kuandika pesa unazotumia kila siku, unaweza kulinganisha na bajeti uliyoweka.
  5. Jiepushe na madeni: Ukiwa na madeni, anza kulipa mara moja. Wacha kutumia kadi zako za mkopo na uazimie kufikia lengo lako.
  6. Faidi na mipango ya kuokoa ushuru: Ikiwa kampuni unayoifanyia kazi ina mpango wa kuweka akiba ya kustaafu au mpango mwingine ambao kampuni hukuhifadhia kiwango sawa na kile unaweka, basi jaribu kuweka pesa nyingi iwekenavyo. Kumbuka utakuwa ukiunda shilingi moja (au zaidi) kwa kila shilingi umeweka. Ni nani hapendi pesa za bure! 
2.6
Average: 2.6 (5 votes)
Your rating: None