Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Kwa Nini Bajeti Ni Muhimu

Kama unataka kuanza kuweka akiba, utahitaji kubajeti. Tumia hatua hizi saba ili uweze kufanikisha mpango wako wa fedha.

  1. Anza kuweka hazina mapema iwezekanavyo.
  2. Tegea matarajio yako (mafupi au marefu)
  3. Ambia familia kuhusu kusudi lako la kuweka hazina.
  4. Tengeneza bajeti inayoafikiana.
  5. Angalia huduma iliyo bora na inayokufaa.
  6. Weka mpangilio wako kwa maandishi.
  7. Rejelea mpangilio wako kila baada ya mwezi mmoja au miwili.

Njia bora ya kutengeneza bajeti ya siku za usoni ni kujua vile unavyotumia pesa zako sasa. Kwanza angalia pale pesa zako zinakokwenda na vile zinavyo kuja. Fuatilia mapato yako na matumizi kwa mwezi mmoja kabla haujaunda bajeti. Unahitaji kufuatilia vitu ulivyonunua kutoka kwa kikombe cha chai hadi tikiti ya basi kwa kuzinakili katika kijitabu au kuweka risiti. Nakili matumizi kwa kila kitengo kila mwezi. Usisahau kuongeza pesa zile unazohifadhi kila mwezi kukusaidia katika malengo yako ya usoni. Kuwa mkweli katika bajeti yako. Bajeti huwa ni mwanzo tu. Mpango wako hautakuwa na maana mpaka ujifunze kujenga thamani yako, weka akiba na kuwekeza kwa namna.

 

 

0
No votes yet
Your rating: None