Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Mbinu za kueneza umuhimu wa maziwa ya mbuzi

  • Kuelimisha watu kuhusu umuhimu wa maziwa ya mbuzi na iwapo umefuga mbuzi washauri wenzako kuonja na kutumia maziwa haya
  • Watafute wenzako wanaofuga mbuzi wa maziwa na muungane kubuni chama ama makundi ya kutetea haki zenu kama wakulima ili kuimarisha ufugaji huu kama vile kupigania kulipwa bei nzuri kwa maziwa ,kuundwa kwa soko bora la bidhaa hii, ama njia bora za kuboresha kilimo hiki.
  • Mkiwa kwenye makundi haya piganieni kwa pamoja kubuniwa kwa soko ama kiwanda cha maziwa ya mbuzi kama vile mwaweza kuzungumza na kiwanda cha KCC kinachonunua maziwa ya ng’ombe ili pia kianze kununua maziwa ya mbuzi au mbuniwe kiwanda chenu cha maziwa hayo.mkiwa kwenye makundi hayo mwaweza kuunganisha shamba ama vipande vyenu vya ardhi ili kuwa na ardhi ya kutosha ya kufuga mbuzi hawa na ili kuufanisha mradi huu.mbunu hii imetumika katika kilimo cha majani chai na imefanikiwa hivyo basi pia yaweza kufaulu katika ufugaji wa mbuzi.
  • Tafuta ushauri ama msaada kutoka kwa taasisi za utafiti wa mifugo kuhusu uwezekano wa kupata chakula cha mbuzi cha hali ya juu kwa bei nafuu pamoja mbinu nzuri na za kisasa za kufuga mbuzi wa maziwa.
  • Weka mpangilio bora wa kuwachunguza mbuzi wako mara kwa mara ili kutambua mbuzi wagonjwa kwa urahisi na kuwaondoa.
  • Wazalishe mbuzi maziwa wa kienyeji na wale wa kizungu ili kupata aina nzuri ya mbuzi wanoweza kustahimili aina mbali mbali ya hali ya anga.
1
Average: 1 (1 vote)
Your rating: None