Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Nyumba Ya Mbuzi

Unaweza kufuga mbuzi kwa fu ndani ya nyumba ukipenda zero grazing endapo huna shamba kubwa, lakini ikiwa una eneo kubwa la shamba waweza kuwaruhusu wajitafutie nyasi wenyewe.
 
Chumba cha mbuzi mmoja kinaweza kujengwa kwa kutumia mbao na kinapaswa kuwa na kipimo cha upana wa futi 4 urefu wa futi 6 na kwenda juu futi 12 na kumbuka kuacha eneo la futi 6 mraba kwa mbuzi kufanyia mazoezi na ukumbuke kuweka vijisanduku viwili kimoja cha kulia chakula na kingine cha kunywea maji.
 
Ni bora kuhakikisha kuwa mlango wa nyumba ama banda hauangalii moja kwa moja na mahali upepo unatokeapo ili kuwakinga dhidi ya magonjwa yaambukizwayo kupitia hewa.

 

1.5
Average: 1.5 (4 votes)
Your rating: None