Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Mambo muhimu kuhusu ufugaji wa mbuzi wa maziwa

  • Maziwa ya mbuzi ni mazuri na yana madini muhimu kwenye mwili hivyo basi kila mmoja apaswa kujifunza kuyatumia.
  • Ufugaji wa mbuzi wa maziwa ni uwekezaji mzuri haswa kwa wakulima wenye mashamba madogo.
  • Maziwa ni chakula muhimu chenye madini muhimu mwilini na pia ndiyo njia moja wapo ambayo watu huambukizwa magonjwa haswa kwa kupuuza mambo muhimu yanayopaswa kuzingatia.
  • Ukulima ni sawa na biashara na biashara nzuri lazima iwe na mpangilio mzuri haswa kwa matumizi ya pesa zinazoaptikana. Ikiwa hutakuwa na matumizi mazuri ya pesa hizo huenda iwe vigumu kununua vitu muhimu ili kuendeleza biashara hiyo. Hivyo kumbuka kuweka rekodi ili kujua ikiwa unapata faida au hasara na ili kuweza kubaini matatizo yanayokumba biashara yako.
  • Kupitia kwa kuunda makundi ya wakulima ,wakulima hao watafaidika na kupigania kupata bei nzuri ya bidhaa zao pamoja uimarishaji wa sera za serikali ili kuwawezesha kufanya biashara yao chini ya usaidizi mzuri kutoka kwa serikali.
  • Kenya ni mojawapo ya mataiafa yaliyo na watumishi wa umma waliohitimu vizuri katika eneo la afrika mashariki na kati lakini wengi huwa hawawatumii maafisa hawa ipasavo kwani kazi yao kuu ni kukuhudumia.utafaulu ikiwa utatafuta msaada na ushauri kutoka kwa maafisa wa serikali walio kwenye eneo lako.
1
Average: 1 (3 votes)
Your rating: None