Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Umuhimu Wa Afya Ya Umma Kwa Wafugaji Wa Mbuzi Wa Maziwa

Mbuzi wa maziwa sawa na ngombe wa maziwa ndizo baadhi ya njia ambazo magonjwa na maambukizi mengine husambazwa kwa binadamu kupitia kwa maziwa.  Baadhi ya madhara yanayotokana na utumiaji wa maziwa ni kama vile.

Magonjwa

 • Magonjwa kama vile brucellosis na kifua kikuu yanaweza kuambukizwa kupitia maziwa ambayo hayajachemshwa vizuri.
 • Watu wanaweza kuambukizwa magonjwa kupitia kuguza mkojo ama tissue za mnyama aliye mgonjwa ama maji na mchanga palipo na viini vinavyoweza kuambukiza magonjwa haya. Watu wanapaswa kuwa waangalifu wanapoguza mimba za mifugo zilizoharibika.
 • Magonjwa kama vile homa ya matumbo,dysentery na kuendesha yanaweza kuambukizwa kwa kula nyama ambayo haijapikwa vizuri na maziwa yaliyo na bacteria na virusi vinavyoambukizwa magonjwa.
 • Ugonjwa wa kimeta (anthrax) ni ugonjwa hatari unaoambukiza binadamu kupitia hewa, kuguza mzoga wa mnyama aliyekufa ama kula nyama ya mnyama anayeugua ugonjwa huo. Viini vya ugonjwa vyaweza kuishi mchangani kwa miaka mingi na hazikufi kwa urahisi hata ikiwa nyama itachemshwa kwa muda mrefu.
 • Sumu kama vile kuvu au fungus hupatikana katika nafaka zilizooza.Mifugo ikipatiwa aina hii ya nafaka, sumu huingia kwa mwili na yaweza kuambukizwa kwa binadamu anapokunywa au kula nyama ya huyo mnyama. Hivyo basi si vyema kuwapatia mifiggo nafaka iliyooza.
 • Kumbuka kuwa:
  o  Viwango vya dawa inayotumiwa kwa mifugo kuuwa kupe,chawa na viroboto zapaswakuwa vile vilivyoandikwa kwenye dawa wala hupaswi kuzidisha.
  o  Ukizidisha kiwango cha dawa dawa hii hupenya na kuingia ndani ya ngozi.
  o  Matititi na chuchu za mnyama zinapaswa kuoshwa vizuri kabla ya kuanza kukama maziwa baada ya mifugo kutibiwa.
  o  Dawa za mifugo kama vile za kuua minyoo na za kutibu magonjwa zafaa kupewa wanyama kwa kutumia syringe ama kuwadunga sindano.
  o  Mbuzi wafaa kulishwa masalio ya mboga na mimea mingine baada ya kuvuna na ikiwa mkulima hatazingatia kiwango ama wakati wa kuwalisha mbuzi na kuwapa chakula kingi wanaweza kupata wadudu wanaoingia kwenye nyama.
  o  Wakulima wengi huweka kiwango kingi cha dawa kwa nafaka baada ya kuvuna ili kuzuia yasiharibiwe na wadudu na yanapoharibika wao huwalisha mifugo na kuku. nafaka hizi ambazo huwa sumu kwa miili ya mifugo.baada ya kutumia nyama,mayai ama maziwa ya mifugo hawa kiwango kidogo cha sumu hii huingia kwenye miili ya binadamu na kusababisha magonjwa ya mara kwa mara na yasiyotibiki.
  o  Zingatia maagizo ya matumizi yaliyo kwenye chupa na pakiti za dawa.
  o  Tumia kiwango cha dawa kilichopendekezwa kwa mimea wala usizidishe hata ikiwa dawa hiyo haifanyi kazi na badala yake tafuta ushauri kutoka kwa mtaalamu wa kilimo atakayekueleza njia mwafaka au dawa nyingine ya kutumia.
 • Fahamu kuwa dawa za antibiotic zinazosalia:
  o  Dawa hizi hutumiwa na mifugo wagonjwa na ikiwa mnyama ananyonyesha zinaweza kuingia kwa maziwa na kuyafanya kuwa hatari kwa matumizi ya binadamu
  o  Masalio ya dawa hizi za anti biotic pia zaweza kutokana na dawa uliyotumia kutibu ugonjwa wa mastitis hata ikiwa maziwa yanaokena kuwa safi baada ya dawa hiyo kuondolewa,maziwa hayo bado yana kiwango kikubwa cha dawa hiyo
  o   Dawa hizi za anti biotic huwa na maelezo kuhusu muda ambao unapaswa kunywa maziwa ama kula nyama ya mnyama baada ya kumtibu hivyo basi ni bora kuzingatia maagizo hayo na utafute ushauri wa daktari wa mifugo atakayekushauri muda unaopaswa kungoja kabla ya kutumia bidhaa hizi kwa manufaa ya afya yako na y familia yako sawia na watumiaji wa bidhaa zako.
 • Dawa za anti biotic zinazoingia kwenye maziwa ni hatari na zinaweza kusababisha
  o  Allergy ya mara kwa mara
  o  Kuongeza kiwango cha allergy kwa mwili wako
  o  Kusababisha dawa kukataa kufanya kazi ama kutibu magonjwa na hatimaye kusababisha kukosekana kwa dawa za kutibu magonjwa hayo.
   

 

0
No votes yet
Your rating: None