Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Matatizo Yanayowakumba Wafugaji Wa Mbuzi Wa Maziwa Nchini

Wakenya wengi hufuga mbuzi kwa ajili ya nyama na kwa sababu za mila na tamaduni hivyo basi kufanya ufugaji wa mbuzi wa maziwa kubaki nyuma.

Ufugaji huu wa mbuzi hukabiliwa na vizuizi vingi vya utamaduni ambavyo lazima viepukwe ili ufugaji huu uweze kufaulu.

Baadhi ya matatizo yanayokumba ufugaji wa mbuzi wa maziwa ni kama vile:

  • Baadhi ya mila na tamaduni za jamii Fulani hupinga unywaji ama utumiaji wa maziwa ya mbuzi
  • Kufuga mbuzi ndani ya nyumba ni mbinu ya kilimo inayohitaji pesa nyingi na hivyo basi kufanya bidhaa za mbuzi kuhitaji soko lililo tayari na lenye bei nzuri ili kumfaidi mkulima
  • Huwalazimu wakulima wenye eneo dogo la shamba kuwatafutia mbuzi malisho na kununua vyakula vinavyouzwa madukani badala ya kuwafanyia zero grazing jambo linalofanya ufugaji huu kuwa mgumu
  • Mbuzi huzaana kwa njia ya kawaida hivyo basi kuwepo kwa ongezeko la mbuzi hao kuambukizana magonjwa kama vile ugonjwa wa brucella ambao unaweza kuangamiza mbuzi wako.
  • Aina nyingi ya mbuzi huwa wa asili ya maeneo yaliyo na baridi na yale yenye joto kadiri na hivyo basi kuwa vigumu kwa mbuzi hawa kufugwa katika maeneo kame na yenye joto jingi kama vile sehemu za Laikipia,mkoa wa bonde la ufa na kusini mashariki ya mkoa wa kati pamoja na baadhi ya wilaya za nyanda za chini mkoani mashariki

Licha ya matatizo mengi yanayokumba ufugaji wa mbuzi wa maziwa, wakulima wanaotaka kufuga mbuzi lazima washirikiane kueneza umuhimu wa maziwa ya mbuzi na kuyafanya yatambulike.

0
No votes yet
Your rating: None