Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Aina za sungura

Mfugaji anahitaji kutambua sungura ambao atatumia kama mbegu kwa kuzalisha wengine wa hali ya juu. Ni vyema kutenga sungura wangali wadogo wakiwa miezi minne kwa wa kike na miezi sita kwa sungura wa kiume yaani kabla hawajaanza kuzaa. Baada ya kupandisha kwa mara ya kwanza na wanapopata mimba sungura hao wa kike ni vyema kuwatenga na kuwaweka katika chumba chao maalum ili kuanzisha kizazi kingine.

Kuna aina mbali mbali wa sungura lakini wanagawanywa mara mbili kwa matumizi. Moja ni kwa matumizi ya ngozi yake kwa kutengeza kofia, mifuko, na mishipi na pili kuna aina ya sungura ambao hufugwa kwa kuzalisha nyama. Mfano wa aina ya sungura wa ngozi ni “Angora” ambaye manyoa yake ni marefu. Na kwa sungura wanaofugwa kwa nyama ni aina ya sungura ambao hukua haraka, uzito wa sungura wa nyama ni kutoka kilo mbili hadi kilo tano. Bw. Wachira anafuga sungura anina ya Califonia White na Newzealand White, Chinchila Flemish Giant ambaye ni mkubwa, an pia hufuga sungura aina ya Flemish Fender.

2.5
Average: 2.5 (8 votes)
Your rating: None