Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Hatua Saba za Kununua Nyumba

Kununua nyumba kwa mara ya kwanza kwaweza kukawa kwa kukufurahisha na pia kwa kuogofya. Kuna mambo chungu nzima ambayo wapaswa kuyafikiria, ilhali baadhi ya hayo mambo hujajipanga sambamba. Huu mwelekeo wa haraka utakufanya uhisi kana kwamba wakifahamu kile unachokifanya.

Hatua ya kwanza: Panga bajeti. Yawezekana kwamba utahitaji dhamana kuilipia nyumba yako. Fanya hesabu kwa kina kabla hujaenda kutafuta nyumba, ni kiwango kipi cha pesa utakachoweza kulipia hiyo dhamana kila mwezi? Yaenda utahitaji kuweka amana, lakini ikiwa unanunua nyumba mara ya kwanza, unaweza pata mkopo unaotoshanan na bei ya nyumba. Kwa hivyo usipoteze wakati ukiangalia nyumba huwezi kumudu kulipa.  

Hatua ya pili: Fanya uamuzi kuhusu kule unakotaka kununua nyumba: Uamuzi huu utategemea bajeti yako. Kumbuka ni heri kununua nyumba iliyo ndogo zaidi katika mazingara mazuri kuliko kununua nyumba kubwa zaidi mahali pabovu.

Hatua ya tatu: Anza kutafuta. Waweza kuwatembelea maajenti wa nyumba katika eneo hilo ili wakuonyeshe nyumba zilizo katika kimo chako cha bajeti. Pia waweza kuangalia magazetini ili upate habari kuhusu nyumba zinazouzwa katika sehemu hiyo. Ni wazo zuri pia kutembelea majumba ya maonyesho ambako waweza ukapata wazo jinsi nyumba zilivyo na hata ukapata nyumba yako unayotaraji.

Hatua ya nne: Elezea madhumuni. Punde unapopata nyumba iliyosawa kwa bei nzuri, basi ni wakati wa kueleza madhumuni yako. 

 
Hatua ya tano: Chukua dhamana. Iwapo utaenda kwenye benki au kampuni ya mikopo ya ujenzi au utapitia kwa ajenti wa dhamana, hakikisha umetafuta viwango vizuri na malipo yatakayokuwa rahisi kumudu.

Hatua ya sita: Uhamisho wa stakabadhi. Muda wa uhamisho waweza kuwa mkubwa kidogo na hapa ndipo kuna malipo mengi ambayo hukutarajia hutokea. Unaposubiri hili kutendeka, waweza kwanza kutuma barua za 'ubadili wa anwani' kwa wadeni, kampuni za bima na watu wengine ambao watahitaji kujua anwani yako mpya. Pia waweza kufanya mpango ili laini yako ya simu ihamishwe au ufunge akaunti.

Hatua ya saba: Ingia katika nyumba! Uwe umeenda kwenye afisi za baraza la mji ili kufanya mipango ya mapema ya kubadilisha majina ya mlipaji wa stima na maji hadi kwa jina lako au hata kufungua akaunti iwapo wauzaji hawatakuwachia. Waweza pia ukataka kufanya mipango ya kujipatia laini ya simu au ile iliyoko iandikwe upya kwa jina lako. Tafuta kampuni ya kukusaidia kuhama na ufanye mpango ni nani atakaye watunza watoto wako siku ya kuhama.
2
Average: 2 (2 votes)
Your rating: None