Skip to Secondary Navigation Skip to Main Content

Current Domain

Languages

Katika sehemu hii

Jinsi ya kutuma pesa kupitia Benki

Unaweza kuweka pesa moja kwa moja kwa akaunti ya mtu mwingine bora uwe na maelezo kamili kumhusu. Hivi utakuwa umeokoa pesa ungelipia kutuma kwa njia zingine. Hizi hapa ni njia zingine unazoweza kutumia kupitia kwa benki:-

  1. Jua kiasi cha pesa unachotaka kutuma.
  2. Utahitaji jina la mtumiwa (jina la akaunti yake), benki yake, namba ya tawi na namba ya akaunti. Utahitaji kujua aina ya akaunti aliyo nayo; ni ya akiba au ni ya hundi?
  3. Unaweza kutoa pesa kwenye akaunti yako ama uandike hundi kwa kiasi cha pesa unachotuma. (Kumbuka, hundi itakuwa na gharama ya juu). Halafu utaenda kwa tawi lililo karibu la benki ya unayemtumia, na uiweke moja kwa moja kwa akaunti yake. Au uende kwa benki yako uwaulize watoe pesa kutoka kwa akaunti yako na kuiweka moja kwa moja kwa akaunti ya yule unatumia.  Njia yako ya tatu ni kutuma pesa kwa akaunti ya unayemtumia ukitumia benki yao ya mtandao.
  4. Hakikisha umepata ithibati ya kuweka pesa au kutuma. Kama unatuma kupitia mtandao, omba benki yako ikutumie faksi au barua pepe ili kuhakikisha kuwa anayetumiwa amepokea pesa.

 

 

0
No votes yet
Your rating: None